|
Alisema
uamuzi wa Serikali kuhamia Dodoma hautokani na shinikizo la kisiasa bali ni
utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ambao chimbuko lake ni agizo
lililotolewa Oktoba Mosi, 1973 kwenye Mkutano Mkuu wa 16 wa chama cha TANU.
“Tangu
wakati huo Serikali zote ziliendelea kufanya juhudi mbalimbali za kuandaa
miundombinu na hata awamu ya nne ilisimamia kwa kiwango kikubwa uwekaji wa
miundombinu hiyo,” alisema.
“Pia
tukumbuke kauli ya Mheshimiwa Rais aliyotoa kwenye hotuba yake ya Julai 23,
2016 alipochaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa CCM, na akairudia tena Julai 25,
kwenye maadhimisho ya kumbukumbu ya Mashujaa na mimi siku hiyo hiyo nikaweka msisitizo,”
alisema.
Alisema
uamuzi wa Serikali ya awamu ya tano wa kuhamia Dodoma unakuja baada ya
kuridhishwa na ujenzi wa miundombinu na maeneo ya kutolea huduma za kijamii kwa
wageni na wenyeji ikiwemo Hospitali ya Benjamini Mkapa iliyopo katika Chuo Kikuu
cha Dodoma (UDOM) yenye uwezo wa kutibu magonjwa makubwa kama ya moyo na figo.
Waziri Mkuu
alisema tayari Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma (CDA) ina mpango
kamambe (master plan) na ina viwanja vya kutosha kujenga makazi na ofisi
mbalimbali.
IMETOLEWA
NA:
OFISI YA
WAZIRI MKUU
|
No comments:
Post a Comment