Taswira Picha Katika Kupatwa kwa Jua Nchini Tanzania Leo Septemba 01,2016. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, September 01, 2016

Taswira Picha Katika Kupatwa kwa Jua Nchini Tanzania Leo Septemba 01,2016.


Wananchi kutoka maeneo mbalimbali wakiwa wamekusanyika kushuhudia  tukio la kupatwa kwa jua leo Septemba 01,2016 ambapo Watalii na wana Anga kutoka mataifa mbalimbali duniani wakiwemo wanafunzi wa shule wameungana kushuhudia tukio hilo kubwa na la kihistoria la kupatwa kwa jua katika Kata ya Rujewa wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya.

Hii itakuwa ni mara ya kwanza Tanzania kutokea tukio hilo tangu Aprili 18, 1977 na kwamba tukio kama hilo la kihistoria linatarajiwa kutokea tena nchini Mei 21, 2031.


Mbali ya kata ya Rujewa ambako wameshuhudia kupatwa kwa jua kwa asilimia 97 sawa na miji ya Makambako, Masasi, Mbeya, Tunduru, Njombe na Sumbawanga, miji mingine ambayo itaona tukio hilo kwa ukaribu zaidi wa asilimia 96 ni Katavi, Nachingwea na Songea ikifuatiwa na Kigoma, Iringa, Mtwara na Lindi.


Tukio hili la kupatwa kwa jua katika eneo hilo la Kata ya Rujewa litatokea leo kuanzia majira ya saa 4:17 asubuhi ambapo eneo hilo litaonekana kwa asilimia 90 hadi umbali wa kipenyo cha kilometa 100.


Ikumbukwe kuwa tukio kama hilo la kupatwa kwa jua lilitokea Julai 31,1962 takribani miaka 50 iliyopita na tukio lingine lilitokea Aprili 18, 1977, na wataalamu wa anga wanabainisha kuwa tukio kama hilo litatokea tena hapa nchini Mei 21, 2031.



Ili kuweza kutazama tukio hilo la kupatwa kwa jua kwa uzuri zaidi wataalamu wa anga wameeleza kuwa tayari wamefanya maandalizi ya vifaa maalumu kwa ajili ya tukio hilo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad