|
Mjukuu wa
Mzee Gotho aitwaye Suryanto ameeleza kuwa kwa mujibu wa nyaraka za serikali,
babu yake huyo alizaliwa katika Kisiwa cha Java ya Kati mnamo Desemba 31 mwaka
1870 na kuongeza kuwa mpaka sasa bado anaendelea kuvuta sigara ingawa umri wake
ni mkubwa (miaka 145).
|
|
Mbali na
mjukuu wake huyo, ofisa mmoja wa Serikali naye alithibitisha umri wa mzee Gotho
kwa kusema, “Tunaamini stakabadhi hizi ni halali, kwa mujibu wa nyaraka rasmi
za serikali. Tunaamini tarehe yake ya kuzaliwa ni sahihi,” anasema Afisa wa
Serikali Wahyu Wiyanto.
Akihojiwa na
BBC, mzee Gotho alisema, “Huwa najaribu kuwa mvumilivu na kuamini kuwa kuna
watu watakaonitunza, nimeishi muda mrefu kwa sababu nina watu wanaonipenda na
kunitunza.”
|
|
Serikali ya
Indonesia ilianza kunakili rasmi kuzaliwa kwa watu miaka ya 1900, hivyo ni
vigumu kuthibitisha tarehe kamili ya watu waliozaliwa kabla ya hapo.
Katika jamii
ambayo Mbah Gotho anatoka, wenyewe humchukulia kama shujaa wao huku akiwa
ametunza kumbukumbu ya matukio makubwa yaliyowahi kutokea enzi za ukoloni na
maisha yake kwa ujumla.
|
|
“Siku ya
Uhuru alikuwa akialikwa kusimulia yaliyotokea wakati wa vita. Anaweza kusimulia
kuhusu vita dhidi ya wakoloni kutoka Japan na Uholanzi,” anasema Wahyu Wiyanto.
Mjukuu wake
anasema mzee huyo huwa hana masharti mengi na huwa halazimishi kupewa chakula
maalum kama walivyo vikongwe wengine.
“Kitu pekee
alitutaka tufanye ni kununua jiwe la kaburi lake,” anasema.
Mzee huyo
anasema kwa sasa anaishiwa na nguvu na hatarajii Kuishi miaka mingi
zaidi ijayo.
“Sina nguvu
kama zamani. Hata kutembea ni shida. Nilikuwa mkulima na nilivua samaki mtoni.
Sitaki kuendelea kuishi sana, ndio maana nimeandaa kaburi. “Ili nikifariki,
kila kitu kiwe tayari,” anasema Gotho.
“Kwa sasa
nataka tu kufariki, lakini wakati wangu haujafika bado.”
Mtu ambaye
aliishi miaka mingi zaidi duniani kulingana na Guinness ni Jeanne Calment
kutoka Ufaransa ambaye aliishi miaka 122 na siku 164 . Aliaga dunia mwezi
Agosti mwaka 1997.
|





No comments:
Post a Comment