Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
(NIDA) itaanza kutoa Vitambulisho vipya vya Taifa vyenye saini kwa wananchi
wote waliokamilisha taratibu za usajili na utambuzi na kuchukuliwa alama za
kibaiolojia (Alama za vidole, Picha, Saini ya Kielektroniki).
Kwa mujibu wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu
wa NIDA Bw. Andrew Massawe; utekelezaji wa zoezi hilo utaanza rasmi Jumanne
tarehe 14 Septemba 2016 , katika ofisi zote za NIDA zikiwemo ofisi za Wilaya
zilizoanza usajili Tanzania ,Zanzibar na mikoa ya Dar-es-salaam, Pwani, Lindi,
Mtwara, Morogoro, Tanga, Arusha, Kilimanjaro, na Ruvuma) pamoja na waheshimiwa
Wabunge Dodoma.
Kwa sasa vitambulisho vya Taifa
vimeanza kutumika katika baadhi ya huduma nchini hususani kwenye mabenki kwa
ajili ya kufungua akaunti na kuthibitisha taarifa za mtu kabla ya kupatiwa
huduma. Taratibu za kupanua wigo wa
matumizi ya Vitambulisho kielektroniki kwa kushirikiana na Taasisi mbalimbali
zinaendelea.
|
No comments:
Post a Comment