|
Afisa mkuu
mtendaji wa Apple Tim Cook alizindua iPhone 7 katika Jimbo la California,Nchini Marekani.
Kampuni ya
Apple imethibitisha kwamba simu yake mpya ya iPhone haitakuwa na tundu la
kawaida la kifaa cha kusikiza sauti, ambacho kwa Kiingereza hufahamika kama
headphone.
Simu hiyo ya
iPhone 7 badala yake itatumia teknolojia ya Apple ya lightning, ambayo
itawezesha mtu kutumia tundu moja kuunganisha simu na vifaa vingine.
Apple pia
watavumisha kutumiwa kwa visikizia sauti ambavyo havitumii nyaya, na imetoa
aina yake ya earphone zinazojulikana kama Airpods.
Kampuni hiyo
imesema imehitaji kutumia ujasiri kuchukua hatua hiyo.
Hata hivyo,
hatua hiyo huenda ikawaudhi baadhi ya wateja ambao sasa watahitajika kununua
kifaa unganishi yaani adapter ndipo waweze kutumia visikizia sauti.
Kampuni hiyo
ya Marekani ilizindua simu hiyo yake mpya katika hafla mjini San Francisco,
Marekani.
Hii imejiri
baada ya kipindi cha mwaka mmoja cha kushuka kwa mauzo ya simu za iPhone na
kupungua kwa sehemu inayodhibitiwa na kampuni hiyo sokoni.
Sifa
nyingine:
- kitufe cha nyumbani sasa kinaweza
kutofautisha uzito kinapobonyezwa na kutoa mtikisiko. Kitufo hicho sasa
hakiingii ndani ya simu.
- simu hizo zinaweza kuingizwa ndani ya maji
ya kina cha 1m (3.2ft) kwa dakika 30 wakati mmoja bila kuharibika.
- aina kubwa ya iPhone 7 Plus ina lensi mbili
za kamera sehemu ya nyuma, ambayo inaimarisha uwezo wa kupiga picha.
Uzinduzi wa
simu hizo umetokea siku chache baada ya Tume ya Ulaya kuamua Apple inafaa
kulipa €13bn (£11bn) kama malimbikizi ya kodi kwa Ireland, uamuzi ambao Apple
imekata rufaa.
|
No comments:
Post a Comment