Watu watatu
wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wanadaiwa kukamatwa na polisi wakiwa na zana
mbalimbali ambazo hutumiwa na vyombo vya ulinzi zikiwamo silaha za vita na sare
za polisi.
Vitu hivyo
vinadaiwa kutumiwa na watu hao kufanya
ujambazi.Inadaiwa kwamba watu hao ni wale waliovamia na kuiba fedha
katika jengo la Sophia House lililopo Keko
Dar es Salam wakiwa wamevaa sare za polisi na kutumia gari ya Noah.
Taarifa kutoka chanzo cha kuaminika zinaeleza kwamba
watu hao ni pamoja na mwanamke mmoja aliyekamatiwa Bunju
katika Manispaa ya Kinondoni ambako vilikutwa vitu vyote vilivyoporwa na
wanaume wawili waliokamatiwa Mbagala
Manispaa ya Temeke, Dar es Salaam.
Chanzo hicho
kilieleza kwamba silaha zilizokamatwa ni
pamoja na bunduki tatu za SMG na risasi zake 260, bastola 16 na risasi zake
526, panga moja na michimbiko mitatu ya kung’olea mageti..
Vitu vingine
ni pingu za chuma 45 na tatu za
plastiki, ‘radio call’ 12 , kamera ya
CCTV moja, gari moja ya Noah, sare ya
polisi jozi moja, ‘pump action tatu na mkasi mmoja.
|
No comments:
Post a Comment