Watahiniwa
795,761 wanatarajia kufanya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi (PSLE)
unaofanyika leo na kesho nchini kote.
Akizungumza
Dar es Salaam jana Septemba 06,2016, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la
Taifa (NECTA), Dk Charles Msonde alisema wanafunzi 372,883 ambao ni sawa na
asilimia 46.86 ni wavulana na wasichana ni 422,878 ambao ni asilimia 53.14.
Mwaka 2015
watahiniwa waliosajiliwa kufanya mtihani walikuwa 775,729 huku 763,602 ndio
waliofanya mtihani huo na wanafunzi 518,034 walifaulu.
Dk Msonde
alisema watahiniwa 765,097 watafanya mtihani kwa lugha ya Kiswahili na
watahiniwa 30,664 watafanya mtihani kwa lugha ya Kiingereza ambayo wamekuwa
wakiitumia katika kujifunzia. Masomo yatakayotahiniwa ni Kiswahili, Kiingereza,
Sayansi, Hisabati na Maarifa.
Alisema
watahiniwa wasioona waliosajiliwa kufanya mtihani ni 95 wakiwemo wavulana 57 na
wasichana 38 wakati wale wenye uoni hafifu ambao huhitaji maandishi makubwa ni
810 ambao kati yao wavulana ni 402 na wasichana ni 408.
“Maandalizi
yote kwa ajili ya mtihani huo yamekamilika kiwa ni pamoja na kusambazwa kwa
karatasi za mitihani, fomu maalum za kujibia mtihani na nyaraka zote muhimu
katika halmashauri na manispaa zote nchini,” alisema Dk Msonde.
Aidha, Dk
Msonde alitoa mwito kwa kamati za mitihani za mikoa na halmashauri kuhakikisha
taratibu za mitihani ya Taifa zinazingatiwa ikiwa ni pamoja na kuhakikisha
mazingira ya vituo vya mitihani yanakuwa salama, tulivu na kuzuia mianya ya
udanganyifu.
“Wasimamizi
wanatakiwa kusimamia kwa umakini na uadilifu wa hali ya juu. Nawaaasa
kujiepusha na vitendo vya udanganyifu kwani Baraza litachukua hatua kali kwa
yeyote yule atakayebainika kukiuka taratibu za uendeshaji wa mitihani ya
Taifa,” alieleza.
CHANZO: HABARI LEO.
|
Wednesday, September 07, 2016
795,761 kufanya mtihani darasa la 7 leo Septemba 07,2016.
Tags
# HABARI
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
HABARI
Labels:
HABARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment