Ligi kuu Soka Uingereza 2016/2017 - Taswira Picha Guardiola 1-0 Mourinho. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, September 10, 2016

Ligi kuu Soka Uingereza 2016/2017 - Taswira Picha Guardiola 1-0 Mourinho.

Kocha Pep Guardiola, Manchester City wamefanikiwa kuwatuliza mashetani wekundu Manchester United kwa mabao 2-1 katika mchezo uliopigwa kwenye dimba la Old Trafford mchana wa leo Septemba 10,2016.


Man City waliotawala mchezo huo kwa kiasi kikubwa walifanikiwa kupata bao la kwanza kupitia kwa Kelvin de Bruyne akimalizia kwa ufasaha pasi ya straika wa Nigeria, Kelechi Iheanacho dakika ya 15.

Wakati United wakiendelea kutafuta bao la kusawazisha, Iheanacho ambaye alifunga bao pekee katika mchezo wa kimataifa kati ya Nigeria dhidi ya Taifa Stars aliipatia bao la pili Man City dakika ya 36 akitazamana na kipa baada wachezaji wengine kudhani ameotea.
Dakika tatu kabla timu hazijaenda mapumziko, Zlatan Ibrahimovic aliipatia Man United bao la kufutia machozi baada ya kipa wa Man City kupangua mpira na kumkuta mfungaji.

Kwa matokeo haya Man City imebaki kileleni kwa kufikisha alama 12 ikifuatiwa na Chelsea yenye pointi 9 sawa na Man United.




No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad