|
Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati
ya Yanga SC dhidi ya Majimaji unachezwa leo ,Septemba 10,2016 kwenye Uwanja wa
Uhuru jijini Dar es Salaam na Yanga SC inaondoka
na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Majimaji.
Mfungaji bora wa Ligi Kuu msimu
uliopita, Amissi Joselyn Tambwe alifunga mabao mawili kipindi cha pili baada ya
kiungo Deus David Kaseke kutangulia kufunga kipindi cha kwanza.
Yanga sasa inafikisha pointi saba,
baada ya kucheza mecni tatu, ikishinda mbili na sare moja – sawa na mahasimu
wao, Simba SC.
Mechi nyingine za Ligi Kuu leo,Jumamosi-
Mwadui FC imelazimishwa sare ya 2-2 na ndugu zao Stand United Uwanja wa Mwadui
Complex, Shinyanga, Mbeya City imefungwa nyumbani 2-1 na Azam FC na Ndanda FC
imelazimishwa sare ya 0-0 na Kagera Sugar, Ruvu Shooting imewalza ndugu zao JKT
Ruvu 1-0 Uwanja wa Mabatini, Mlandizi Pwani.
LIGI KUU VODACOM -2016/2017.
Jumapili Septemba 11, 2016.
Simba SC v Mtibwa Sugar
Tanzania Prisons v Toto Africans
Jumapili Septemba 12, 2016.
African Lyon v Mbao FC
|
No comments:
Post a Comment