|
Polisi
wamewatia mbaroni watu watano wanaodaiwa kusambaza taarifa kwenye mitandao
ya jamii kuwa Mbunge wa zamani wa Moshi
Mjini, Philemon Ndesamburo amefariki dunia.
Miongoni mwa
waliokamatwa na kuhojiwa na polisi na simu zao kushikiliwa kwa uchunguzi, ni
wanachama wa Chadema na maofisa wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro
(Kia).
Kamanda wa
Polisi Mkoa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa
jana alisema kuwa, uzushi huo kuwa Ndesamburo amefariki dunia,
ulisambazwa zaidi kupitia makundi ya WhatsApp.
“Tarehe
29/7/2016 mzee Ndesamburo alifika polisi na kutoa taarifa kuwa katika mitandao
ya jamii kuna taarifa na picha yake, inasambazwa kwa kasi kuwa amefariki
dunia,” alisema Mutafungwa na kuongeza:
“Picha hiyo
ilikuwa na maneno RIP (Rest in Peace), wakimaanisha apumzike kwa amani.
Tulifungua jalada na kitengo chetu cha Cyber Crime (makosa ya kimtandao)
kiliingia kazini.”
Alisema watu
mbalimbali walihojiwa na polisi wanaendelea kazi hiyo pia watu watano walikiri
kupokea ujumbe huo na kuusambaza.
Kamanda
Mutafungwa alisema wanaendelea na uchunguzi wa kisayansi kumpata mtu
aliyeanzisha ujumbe huo, ambao ulisababisha usumbufu kwa Ndesamburo na familia yake.
Wanaoendelea
kuhojiwa ni Ofisa Usalama wa Kampuni ya Kilimanjaro Airport Development (Kadco)
na msimamizi wa waongoza ndege wa Fast Jet Uwanja wa Kia.
Wengine ni
wanachama watatu wa Chadema, ambacho Ndesamburo ni Mwenyekiti wake wa Mkoa
Kilimanjaro. Katibu wa Chadema Mkoa Kilimanjaro, Basil Lema alithibitisha
kuhojiwa kwa wanachama wake na kwamba, anaamini mwanzilishi wa taarifa hiyo ya
uzushi hajakamatwa.
|
No comments:
Post a Comment