TASWIRA PICHA:- Rais Magufuli atua Mkoani Mwanza kwa Ziara ya Siku mbili. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, August 10, 2016

TASWIRA PICHA:- Rais Magufuli atua Mkoani Mwanza kwa Ziara ya Siku mbili.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia mamia ya wakazi wa Sengerema mkoani Mwanza mara baada ya kuwasili kwa ziara ya siku mbili kuanzia Leo Agosti 10 na 11,2016 akitokea Chato mkoani Geita.

Rais Magufuli ataitimisha ziara yake Agost 11,2016 kwa kukagua ujenzi wa daraja la watembea kwa miguu la Furahisha Jijini Mwanza, pamoja na upanuzi wa barabara ya Furahisha hadi Pasiansi ambapo ataweka jiwe la msingi katika ujenzi wa miundombinu hiyo.

Rais Magufuli atahutubia wananchi baada ya kukagua miradi hiyo ya ujenzi katika mkutano wa hadhara utakaofanyika kuanzia majira ya saa nanne mchana katika uwanja wa Furahisha.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella mara baada ya kuwasili katika Wilaya ya Sengerema Mkoani Mwanza.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia wanakwaya wa UWT Kisima cha maji Chumvi mara baada ya kuhutubia wakazi wa Sengerema mkoani Mwanza.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwalimu Mstaafu wa Shule ya Sekondari Sengerema Wilson Fumbuka Mbanga ambaye walifundisha naye shule hiyo tokea mwaka 1982-1985 mara baada ya kumaliza mkutano wa hadhara Sengerema Mkoani Mwanza.
 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiaagana na wakazi wa Sengerema mkoani Mwanza mara baada ya kumaliza kuwahutubia.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Busisi wakati akielekea Mwanza.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa ndani ya kivuko cha MV. Misungwi wakati akielekea mkoani Mwanza. 

PICHA NA IKULU.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad