|
Mamlaka ya
Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) imevipa onyo na kuvipiga faini vituo
viwili vya televisheni na kimoja cha redio kwa kukiuka maadili ya utangazaji.
Vituo hivyo
ni ITV, Clouds Tv na Clouds Fm Radio, vyote vya jijini Dar es Salaam, ambavyo
kwa ujumla vimepigwa faini ya Sh milioni 19.
Akitoa
uamuzi uliofikiwa na Kamati ya Maudhui ya TCRA, Makamu Mwenyekiti wa Kamati
hiyo, Joseph Mapunda alisema vituo hivyo vilibainika kukiuka Kanuni za Huduma
za Utangazaji na kuvitaka kuwa wasimamizi wazuri wa vipindi vyao.
Mapunda
alisema kamati hiyo imekipa onyo na kukipiga faini ya Sh milioni 10 kituo cha
televisheni cha ITV kwa makosa mawili; la kwanza ni kupitia kipindi chake cha
Kumekucha cha Juni 15, mwaka huu,2016 kati ya saa 1:00 na 1:30 asubuhi ambacho
mtangazaji alifanya mahojiano na Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa
kuhusu mwenendo wa Bunge la Bajeti, na Mchungaji Msigwa alitamka maneno ya
kashfa dhidi ya Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson.
“…mtangazaji
hakuchukua jitihada za kumwomba Mheshimiwa Peter Msigwa kufuta lugha ya matusi
aliyoitumia, bali alionekana akifurahia na kuendelea kumuuliza maswali
mengine,” alisema Mapunda.
Katika kosa
la pili, Mapunda alisema kituo hicho kilikiuka kanuni katika taarifa ya habari
ya Juni 23,2016 kati ya saa 1:00 na 2:00 asubuhi, kilitangaza taarifa ya msichana wa
miaka 16 aliyebakwa na kupewa ujauzito na walitumia utambulisho wa msichana
huyo kwa jina na shule anayosoma.
Katika
utetezi wake, Mwakilishi wa ITV, Stephen Chuwa alikiri kuwa Mchungaji Msigwa
alitoa maneno ya kashfa na hakutembea katika ahadi yake ya kutomkashifu mtu.
Aidha
alisema kama mtangazaji angemuomba kufuta kauli, mjadala ungekuwa mkubwa zaidi.
Alisema watachukua hatua za kumwomba radhi Dk Tulia kutokana na kashfa hiyo.
Kwa upande
wa Kituo cha Clouds Tv, kituo hicho kimepewa onyo na kupigwa faini ya Sh
milioni nne ambazo wanapaswa kulipa ndani ya siku 30 kuanzia siku ya hukumu.
Mapunda
alisema kituo hicho kupitia kipindi chake cha Hip Hop, kilichorushwa kati ya
saa 8:00 mchana na 12:00 jioni, kilirusha video ya nyimbo za Asanteni kwa Kuja
wa Mwana FA na Break It Down wa Lil Bebbie, ambazo zinadhalilisha utu wa
mwanamke.
Aidha,
Clouds Fm pia imepewa onyo na kupigwa faini ya Sh milioni tano kwa vipindi
vyake vya ‘Power Breakfast’ na Jahazi kwa walikiuka kanuni za utangazaji.
Alisema
katika kipindi cha Jahazi cha Mei 9, kilichorushwa kati ya saa 10:00 hadi 12:55
jioni, watangazaji walisikika wakishabikia taarifa ya mtu kufanya ngono na
mbuzi, ambako walieleza kuwa mtu huyo na mbuzi ni kama mtu na mpenzi wake,
jambo lililoonesha wanahamasisha vitendo hivyo.
Aidha, Mei
18, mwaka huu katika kipindi cha Power Breakfast, kilichorushwa kati ya sa
12:00 na 4:00 asubuhi baada ya kusoma taarifa ya Hospitali ya Taifa Muhimbili
kuhusu kupandikizwa kwa sehemu za siri za kiume kwa mtoto wa miaka mitatu,
aliyezaliwa akiwa hana na kulelewa kama mtoto wa kike.
|
No comments:
Post a Comment