MKUSANYIKO WA PICHA:-Jeshi la Zimamoto na Uokoaji –Bukoba, mkoani Kagera likitoa elimu ya kinga na tahadhali ya moto wilayani Ngara. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, August 11, 2016

MKUSANYIKO WA PICHA:-Jeshi la Zimamoto na Uokoaji –Bukoba, mkoani Kagera likitoa elimu ya kinga na tahadhali ya moto wilayani Ngara.

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji -Bukoba , mkoani Kagera limeendelea Kutoa elimu ya kinga na tahadhali ya moto kwa Makundi mbalimbali ya Jamii, Wafanyakazi wa Taasisi mbalimbali kama vile Radio Kwizera FM,Hospitali ya Halmashauri ya wilaya ya Ngara Nyamiaga DDH , Watumishi wa Huruma Zahanati ,Wafanyakazi wa Moorland Hotel na Wafanyabiashara.

Hapa chini nimekuwekea mkusanyiko wa matukio mbalimbali ya Picha ya Kivitendo wakati Jeshi la Zimamoto na Uokoaji –Bukoba, mkoani Kagera likitoa elimu ya kinga na tahadhali ya moto wilayani Ngara.
Pichani juu na Chini ni Jeshi la Zimamoto na Uokoaji -Bukoba , mkoani Kagera limeendelea leo Agosti 11,2016 Kutoa elimu ya kinga na tahadhali ya moto kwa wanafunzi na staff wa shule ya sekondari lukole iliyopo wilayani Ngara mkoani Kagera ambapo Jumla ya Wanafunzi wapatao 500 wamepata elimu hiyo.
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji -Bukoba , mkoani Kagera limeendelea Kutoa elimu ya kinga na tahadhali ya moto kwa Wafanyakazi wa Hospitali ya Halmashauri ya wilaya ya Ngara Nyamiaga DDH sambamba na Watumishi wa ofisi ya mkuu wa wilaya ya Ngara kwa pamoja na ofisi ya Murugenzi wa Halmashauri ya wilaya.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad