![]() |
|
Wajumbe wa
kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Kahama wakishuhudia wakati wa hafla ya
makabidhiano ya hundi.
|
![]() |
|
Mbunge wa
Kahama Mjini Mhe. Jumanne Kishimba akihutubia wananchi wa Kahama wakati wa
kupokea hundi ya ushuru wa huduma yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni
700.
|
![]() |
|
Meneja Mkuu
wa Mgodi wa Buzwagi,Asa Mwaipopo akiteta jambo na Mkuu wa wilaya ya
Kahama,Fadhili Nkulu wakati wa makabidhiano ya hundi ya malipo ya huduma.
|
![]() |
|
Mkuu wa
wilaya ya Kahama Fadhili Nkulu akihutubia wananchi wa Kahama wakati wa kupokea
hundi ya ushuru wa huduma.
|
![]() |
|
Baadhi ya
wananchi katika wilaya ya Kahama wakishuhudia makabidhiano hayo.
Na Dixo
Busagaga wa Michuzi Blog,Kanda ya Kaskazini.
Mgodi wa
Buzwagi umekabidhi wa halmashauri ya mji wa Kahama hundi yenye thamani ya zaidi
ya shilingi milioni mia saba na kumi na saba (717,276,055/=) ikiwa ni sehemu ya
malipo ya kodi ya huduma(service levy) ambayo hulipwa kwa halmashauri hiyo.
Akizungumzia
malipo hayo ya hundi Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Mhandisi Asa Mwaipopo
amesema kiasi hicho ni malipo ya kuanzia mwezi januari hadi juni mwaka huu.
Mwaipopo
ameongeza kuwa licha ya Kampuni yake kulipa kodi mbalimbali na kujishughulisha
katika kufadhili miradi ya Maendeleo, amesema ipo haja ya Jamii kuilinda na
kuitunza miradi hiyo ili iwe na manufaa kwa Jamii nzima.
“Acacia
kupitia Mgodi wetu wa Buzwagi tunajivunia kuwa wadau muhimu wa maendeleo wa
halmashauli ya mji wa Kahama na serikali kwa ujumla, na tunafarijika sana kwa
ushirikiano ambao tumekuwa tukiupata, ombi letu kwa Jamii zinazonufaika na
miradi yetu kuilinda na kuitunza kwa manufaa ya Jamii nzima.”
Kwa upande
wake Mkuu wa wilaya ya Kahama Mh. Fadhili Nkulu aliyepokea hundi ya kodi ya
huduma kutoka kwa uongozi wa Mgodi wa Buzwagi na baadae kuikabidhi kwa
Mwenyekiti wa halmashauri ya Kahama ameupongeza uongozi wa Mgodi wa Buzwagi kwa
jitihada ambazo wamekuwa wakizifanya katika kuhakikisha wanashirikiana na jamii
katika kutekeleza miradi ya Maendeleo”
Akizungumza
kwa Niaba ya halmashauri ya mji wa Kahama Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Abel
Shija ameupongeza uongozi wa Mgodi na kuahidi kuendelea kushirikiana nao katika
kuiletea Jamii Maendeleo.
|











No comments:
Post a Comment