EPL 2016/2017:-Leicester City wachapwa 2-1 na Hull mechi ya kufungua msimu. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, August 13, 2016

EPL 2016/2017:-Leicester City wachapwa 2-1 na Hull mechi ya kufungua msimu.

Pichani ni Snodgrass amefunga bao la ushindi dakika ya 55.

Mabingwa watetezi wa Ligi ya England Leicester City wameanza msimu wa 2016/17 kwa kuchapwa ugenini na Hull City.

Leicester wamechapwa 2-1, mabao ya Hull yakifungwa na Adama Diomande (46+2') na Robert Snodgrass (55').

Bao la kufutia machozi ya Leicester City limefungwa na Riyad Mahrez kupitia mkwaju wa penalti dakika ya 47.

Matokeo mengine ya ligi kuu ya Uingereza
Leicester City ndio Mabingwa wa kwanza Watetezi kushindwa kushinda mechi ya kwanza ya msimu uliofuata wa 2016/2017 baada ya kutwaa Ubingwa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad