Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkewe Mama
Janeth Magufuli pamoja na Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani, Mbunge wa Sumve Richard Ndassa wakipiga
makofi mara baada ya tukio la uwekaji wa Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Daraja la
waenda kwa miguu la Furahisha pamoja na Upanuzi wa barabara ya Mwanza-airport.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. John Pombe Magufuli ameitaka Wizara ya
Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano kuhakikisha kuwa ujenzi wa daraja la watembea
kwa miguu na upanuzi wa Barabara ya Makongoro jijini Mwanza unakamilika ifikapo
disemba mwaka huu.
Aidha
amesema upanuzi wa barabara ya Makongoro uliokuwa ujengwe kati ya Furahisha
hadi Pasiansi Km 2.8 sasa utaendelezwa hadi kufikia uwanja wa ndege.
Akizungumza
jana,Agosti 11,2016, mara baada ya kuweka jiwe la msingi la daraja la watembea
kwa miguu na upanuzi wa barabara ya Makongoro Mh. Dkt. Magufuli alisema kasi ya
ujenzi wa barabara jijini Mwanza uendane na ujenzi wa uwanja wa ndege ili
kuwezesha mkoa wa Mwanza kuwa kitovu cha nchi za maziwa makuu.
“Nakuagiza
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano
uhakikishe kuwa barabara na daraja la watembea kwa miguu Furahisha
vinakamilika mwezi desemba na mkandarasi wa uwanja wa ndege anaanza kazi mara
moja”. Alisisitiza Rais Dkt. Magufuli.
|
No comments:
Post a Comment