Mkuu wa Mkoa
wa Kagera Mhe. Kijuu Akitoa Taarifa ya Mkoa Kwa Waziri Kairuki..Picha na
Maktaba yetu.
Mkuu wa Mkoa
wa Kagera Mhe. Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu awaagiza viongozi katika
Halmashauri za Wilaya kuchukukua jukumu la kusimamia kikamilifu shughuli mbalimbali
za afya katika Mkao wa Kagera ili kuboresha utoaji wa huduma za afya
kikamilifu katika jamii.
Mhe. Kijuu
alitoa agizo hilo wakati akifungua kikao cha wadau wa afya Agosti 23, 2016
katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
kilichowahusisha Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala wa Wilaya, Wakurugenzi
Watendaji wa Wilaya na Wadau mbalimbali wa Serikali na wasiokuwa wa Serikali
wanaoshirikiana katika kutoa huduma mbalimbali za afya Kagera.
Katika Agizo
hilo Mkuu wa Mkoa alisistiza mambo makuu na muhimu matatu kama ifuatavyo;
Kwanza aliwaagiza viongozi hao kuhakikisha wanajadili kwa kina na kuweka
mikakati ya kutoa huduma ya chanjo
katika Halmashauri za Wilaya ili ziweze kufikia asilimia 95% ya Kitaifa
.
Pili ni
kuhakikisha viongozi wanapitishwa na kuelimishwa kwa undani zaidi na wataalamu
wa afya kuhusu vigezo vilivyotolewa na wafadhili wanaotoa fedha za Busket Fundi
ili kushirikiana katika usimamizi kwenye Halmashauri za Wilaya kukamilisha
mahitaji ya vigezo hivyo ili zikidhi vigezo hivyo na kupata fedha za wafadhili
zikawahudumie wananchi kupitia sekta ya afya.
Mhe. Kijuu
alisema kuwa katika majaribio ya awali yaliyofanyika katika kutathmini vigezo
hivyo ilionyesha kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa ilipata asilimia 93%,
Muleba 83%, Bukoba 14% aidha Biharamulo ilipata asilimia 0% (sifuri) na Halmashauri nyingine kutokana na wataalam
wa afya kutoingiza takwimu za afya katika mfumo wa Wizara ya Afya , Maendeleo
ya Jamii, Jinsia na Watoto.
Mhe. Kijuu
pia aliwakumbusha viongozi hao kuhakikisha wanasimamia na kuchukua tahadhali
zote juu ya kupunguza vifo vya mama na mtoto ambapo aliagiza vituo vyote vya
afya hapa Mkoani Kagera kuanza kutoa huduma za upasuaji wa dharura kwa Halmashauri za Wilaya ambazo hazijaanza
kutoa huduma hiyo zianze mara moja, pia kuimarisha Mfuko wa Afya wa Jamii (CHF)
ili kupata fedha za tele kwa tele.
Naye Mganga
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Dk. Thomas
Rutachunzibwa aliwashukuru wadau wote wa afya wa Mkoa wa Kagera kwa
kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha huduma za afya Mkoani Kagera
zinaimarika na aliwaomba kuendelea na ushirikiano wao mzuri ili kuboresha afya
za wananchi wa Mkoa wa Kagera .
|
No comments:
Post a Comment