Waandishi wa
habari wakichukua taarifa hiyo.
Akizungumza
kwa hisia, CP Mssanzya pia amepiga marufuku
mikutano ya ndani yenye viashiria vya uchochezi na hata ikifanyika
kwenye majukwaa watamshusha muhusika na kumfikisha kwenye mkono wa sheria.
Amesema
Jeshi hilo limebaini kwamba mikutano
hiyo imekuwa ikitumika kuchochea Wananchi na kuwahamasisha kuvunja Sheria za
nchi na kufanya Mapambano na Jeshi la Polisi.
"Kwasababu
hiyo basi,kwa hali ya kutumia mikutano ya ndani kuchochea watu kuvunja sheria
na kupambana na askari, hivyo basi kuanzia sasa jeshi la polisi nchini linapiga
marufuku mikutano yote ya ndani" amesema.
|
Aidha
CP Mssanzya aliwataja Askari waliouawa katika tukio hilo
wakati wakibadilishana lindo kuwa ni
E.5761 CPL Yahya, F.4660 CPL Hatibu, G 9524 PC Tito na G 9996 PC Gastoni
na raia wawili waliojeruhiwa aliowataja kuwa Ali Chiponda na Azizi Yahya wote
wakiwa wakazi wa Mbande.
"Katika
tukio hilo majambazi ambao idadi yao haikufahamika walifanikiwa kupora silaha
mbili aina ya MSG na lisasi 60 na hakuna pesa wala mali ya benki hiyo kuibiwa
au kuharibiwa, ni dhahiri kuwa waharifu hao walikuwa na kusudio moja tu la
kuwashambiulia askari polisi, " alisema.
Alisema
katika hali ya kushangaza baada ya tukio hilo kuna baadhi ya watu waliandika
mitandaoni kubeza na kukeji mazoezi ya kawaida ya Jeshi la Polisi na wengine
waliandika ujembe wa kushabikia tukio hilo la kuuawa kwa Askari Polisi huku
wengine wakidiriki kuandika ujumbe unaosema endapo watapigwa na Polisi
Septemba Mosi, mwaka huu 2016 basi Viongozi wa Jeshi hilo wawaondoe Askari wanaoishi
uraiani na kuwarudisha kambini.
Aliongeza
kuwa Jeshi la Polisi limejipanga vyema kukabiliana na matukio yote ya uvunjifu
wa amani nchini.
|
No comments:
Post a Comment