CAF KOMBE LA SHIRIKISHO:- Yanga SC yaweka uhai matumaini yao finyu ya kusonga Nusu Fainali. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, August 13, 2016

CAF KOMBE LA SHIRIKISHO:- Yanga SC yaweka uhai matumaini yao finyu ya kusonga Nusu Fainali.

Mabingwa wa Tanzania Bara Yanga SC ,Leo Agosti 13,2016 hii kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam wamewatungua Mo Bejaia ya Algeria 1-0 katika Mechi ya Kundi A la CAF KOMBE LA SHIRIKISHO na kuweka uhai matumaini yao finyu ya kusonga Nusu Fainali.

Bao la ushindi la Yanga SC lilifungwa na Amissi Tambwe Dakika ya Pili tu ya mchezo ambao Yanga walikosa Bao kadhaa za wazi.

Yanga SC bado wapo ‘hai’ kusonga Nusu Fainali lakini ikiwa kesho Medeama wataifunga TP Mazembe huko Ghana basi matumaini ndio yamekufa.

Yanga SC bado wapo wakiwa mkiani mwa Kundi A wakiwa na Pointi 4 baada Mechi wakati

Vinara ni TP Mazembe ya Congo DR wenye Pointi 10 wakifuatiwa na MO Bejaia ya Algeria yenye Pointi 5 na Medeama wana Pointi 5.

MSIMAMO.
Yanga SC watacheza Mechi yao ya mwisho hapo Agosti huko Lubumbashi, Congo DR kwa kurudiana TP Mazembe iliyoshinda Dar es Salaam 1-0.

Kundi B limebakisha Mechi 1 tu na tayari FUS de Rabat ya Morocco na ES Sahel ya Tunisia zimeshatinga Nusu Fainali.

CAF Kombe la Shirikisho.

KUNDI A:

-MO Bejaia (Algeria)

-Yanga (Tanzania)                                                                                   

-TP Mazembe (DR Congo)

-Medeama (Ghana)

KUNDI B:

-KAC Marrakech (Morocco)

-Etoile du Sahel (Tunisia)

-FUS Rabat (Morocco)

-Ahly Tripoli (Libya)

MECHI ZA MAKUNDI -RATIBA/MATOKEO:

Mechi za 5

Agosti 12, 2016.

Al-Ahli Tripoli – Libya 1 FUS de Rabat – Morocco 1

ES Sahel – Tunisia 3 KAC Marrakech - Morocco 1

Agosti 13, 2016.

Yanga – Tanzania 1 MO Bejaia – Algeria 0

Agosti 14, 2016.

Medeama – Ghana v TP Mazembe - Congo, DR

Mechi za 6

Agosti 23, 2016.

KAC Marrakech – Morocco v Al-Ahli Tripoli - Libya     

FUS de Rabat – Morocco v ES Sahel - Tunisia  

TP Mazembe - Congo, DR v Yanga - Tanzania 

MO Bejaia – Algeria v Medeama - Ghana

NUSU FAINALI

**Mechi za Kwanza Septemba 16 -18,2016 na Marudiano Septemba 23 - 25,2016.

Mshindi wa 2 Kundi B v Mshindi Kundi A

Mshindi wa 2 Kundi B v Mshindi Kundi A

FAINALI

Mechi ya Kwanza Oktoba 28 - 30,2016 na Marudiano Novemba 4 - 6,2016.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad