![]() | |||
|
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAISTAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
TAREHE 11
JULAI, 2O16
Waziri
wa Katiba na Sheria Mheshimiwa Harrison Mwakyembe anatarajia kufanya ziara ya
kikazi ya siku tatu Mkoani Kagera kuanzia tarehe 14-16 Julai, 2016.
Siku
ya kwanza ya tarehe 14 Julai, 2016 Mhe. Mwakyembe anatarajia kukutana na
kuongea na wadau waliopo chini ya Wizara
yake ya Sheria na Katiba pamoja na Vyombo vya Habari katika Ukumbimbi wa Ofisi
ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera kuanzia saa 6:00 hadi saa 7:00 Mchana. Aidha kuanzia
saa 7:30 hadi 8:30 mchana atatembelea ofisi za RITA kujionea uandikishaji wa
watoto waliochini ya miaka mitano.
Katika
siku ya pili ya tarehe 15 Julai, 2016 Mhe. Mwakyembe atatembelea Gereza la
Wafungwa la Mkoa wa Kagera, Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba na Ofisi ya
Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika Manispaa ya Bukoba ili kuongea na uongozi
wa ofisi hizo ambazo zipo chini ya Wizara yake.
Siku
ya tatu ya tarehe 16 Julai, 2016 Mhe. Mwakyembe akiwa mkoani Kagera ataelekea
Wilayani Biharamulo ambapo atatembelea Gereza la Wafungwa Biharamulo na
kuhitimisha ziara yake katika Mkoa wa Kagera na kuondoka kuelekea Mkoani
Mwanza.
Sylvester
Raphael
Afisa
Habari Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kagera
11
Julai, 2016
|
Monday, July 11, 2016
Home
HABARI
SIASA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI:-Waziri wa Katiba na Sheria kufanya ziara ya kikazi ya siku tatu Mkoani Kagera.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI:-Waziri wa Katiba na Sheria kufanya ziara ya kikazi ya siku tatu Mkoani Kagera.
Tags
# HABARI
# SIASA
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
SIASA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.






No comments:
Post a Comment