ORODHA YA UBORA WA SOKA DUNIANI:-Tanzania yapanda Nafasi 13. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, July 14, 2016

ORODHA YA UBORA WA SOKA DUNIANI:-Tanzania yapanda Nafasi 13.

Shirikisho la soka Duniani FIFA imetoa Orodha ya Ubora Duniani ambapo Argentina wameendelea kushikilia Nafasi ya Kwanza na Mabingwa wapya wa Ulaya Portugal kuzipiku Hispania na Brazil na kushika Nafasi ya 6.

Mbali ya Fainali za EURO 2016 zilizokwisha Jumapili kuwanufaisha Mabingwa Portugal, pia Wenyeji France, Poland, Iceland, Croatia na Wales zimepanda chati.
Nchi ya Kenya imepanda hatua 43 katika orodha ya hivi punde zaidi ya shirikisho la soka duniani FIFA .

Kenya imepanda hatua 43 katika orodha ya hivi punde zaidi ya shirikisho la soka duniani FIFA na kuorodheshwa katika nafasi ya 86 duniani.

Hii ni kwa mujibu wa orodha ya FIFA inayoonesha kuwa Algeria imesalia kidedea barani Afrika japo inaorodheshwa katika nafasi ya 32 duniani.

Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo ndiyo inayoongoza katika kanda ya afrika mashariki na kati.

DR Congo imeorodheshwa katika nafasi ya 59 duniani na 9 barani Afrika.

Uganda Cranes inaorodheshwa katika nafasi ya 15 barani Afrika na nafasi ya 69 duniani nafasi mbili mbele ya vigogo ya soka barani humu Nigeria.
Orodha ya FIFA Tanzania 123.

Kenya ambayo ndilo taifa lililoimarika zaidi inaorodheshwa katika nafasi ya 86.

Harambee stars ya Kenya iliyojifurukuta na kuilaza Congo Brazzaville iliimarika hatua 43 na kuingia chini ya mataifa bora 100 kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miezi sita.

Aidha hii ndiyo nafasi ya juu zaidi kwa Kenya tangu mwaka wa 2008.

Amavubi Stars ya Rwanda imeshuka hatua 8 na kuorodheshwa katika nafasi 111 duniani.

Licha ya kupanda hatua 13, Taifa Stars ya Tanzania inaorodheshwa katika nafasi ya 123

Inafatwa kwa karibu na Burundi ambayo vilevile imepanda hatua 7 na kutimia nafasi ya 125.
Uganda Cranes inaorodheshwa katika nafasi ya 15 barani Afrika na nafasi ya 69 duniani.

FIFA itatoa tena upya Listi ya Ubora Duniani hapo Agosti 11,2016.

Ethiopia ni ya 132,

Sudan 142

Sudan Kusini 153

Mataifa ya mwisho kabisa katika orodha hiyo ya FIFA ni mataifa ya kanda ya Afrika Mashariki yaani Djibouti, Eritrea na Somalia ambazo zote zinaorodheshwa katika nafasi ya 205.
Ufaransa wamepanda Nafasi 10 na kushika Nafasi ya 7 wakati Poland wakipaa Nafasi 11 kuwa wa 16.

Iceland na Croatia zote zimepanda Nafasi 12 na Iceland kushika ya 22 na Croatia kukamata ya 15.

Wales wamepanda Nafasi 15 na kushika Nafasi ya 11 wakati England ikiporomoka Nafasi 2 na kuwa wa 13.

Argentina ingali inaongoza duniani ikifwatwa na Ubeljiji.

Orodha ya mataifa kumi bora barani Afrika

Algeria (32)

Ivory Coast (35)

Ghana (36)

Senegal (41)

Misri (43)

Tunisia (45)

Cameroon (53)

Morocco (54)

DR Congo(59)

Mali (61)

Orodha ya mataifa kumi bora duniani

1 Argentina

2 Ubeljiji

3 Colombia

4 Ujerumani

5 Chile

6 Ureno

7 Ufaransa

8 Spain

9 Brazil

10 Italia

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad