|
Picha ya Pamoja Waziri
na Uongozi wa Mkoa.
Waziri wa Sheria na
Katiba, Dkt Harrison Mwakyembe aliyasema hayo wakati akiongea na wadau
mbalimbali waliopo chini ya Wizara yake, Watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa,
Waandishi wa Habari, Wabunge, Wakuu wa
Wilaya na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe.
Salum M. Kijuu katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa kagera alipowasili Mkoani Kagera leo tarehe
14/07/2016 na kuanza ziara yake ya kazi ya siku tatu.
Waziri Mwakyembe
aliyeongozana na Mkurugenzi wa Mashitaka nchini Bw. Biswalo Mganga na Kaimu
Mtendaji Mkuu wa RITA Bi Emmy K. Hadson alisema katika kikao hicho kuwa ziara
yake mkoani Kagera inalenga mambo makuu
matatu kama ifuatavyo;-
Kwanza ni kufuatilia na
kuhimiza utekelezaji wa sheria
iliyonzishwa mwaka 2011ambayo ilianzisha Tume ya Utumishi wa Mahakama ambayo
ndani yake ilianzisha Kamati za Maadili ya Mahakimu wa Mahakama za mwanzo
katika ngazi ya Wilaya na Kamati za Maadili ya Mahakimu Wakazi na Mahakimu wa
Wilaya katika ngazi ya Mkoa.
Katika kuhimiza
utekelezaji wa sheria hiyo Waziri Mwakyembe aliwaagiza Wakuu wa Wilaya kuunda
Kamati hizo ili kutatua kero za wananchi wanazopata kutoka Makimu wa Mahakama
za Mwanzo ambao wanajifanya miungu watu na kuwanyanyasa wananchi kwa kuwaomba
rushwa na kupindisha haki.
Aidha alimwagiza Mkuu wa Mkoa naye kuunda kamati
hiyo ya mkoa ili kutatua kero za malalamiko kwa Mahakimu Wakazi na Makimu wa
Wilaya.
Kamati hizo za Maadili
katika ngazi ya Wilaya wajumbe wake ni Mkuu wa Wilaya ambaye ni mwenyekiti wa
Kamati hiyo, Katibu Tawala wa Wilaya ni katibu wa kamati hiyo, Mkuu wa Wilaya
pia atateua kiongozi mmoja katika Wilaya husika na Mwananchi mmoja anayeheshimika
katika jamii nao watakuwa wajumbe wa kamati hiyo pamoja na Hakimu Mfawidhi wa
Wilaya naye ni Mjumbe.
Pili, Waziri Mwakyembe
alisema katika ziara yake Mkoani Kagera ni kuhimiza juu ya uchukuaji
na utunzaji wa takwimu za vizazi na vifo hasa kwa watoto wadogo.
Waziri Mwakymbe alisema kwa nchi nzima ya
Tanzania uandikishaji wa takwimu za vizazi na vifo bado ni tatizo kubwa kwani katika
Tanzania watoto na watu wazima takwimu zinaonyesha kuwa wenye vyeti vya
kuzaliwa nia asilimia 11% tu.
“Tatizo lilionekana
kuwa kubwa baada ya Serikali kuamua kutoa elimu bure hapo ndipo ilionekana kuwa
mfumo wetu wa takwimu una matatizo makubwa kwani watoto walifumuka sana kiasi ambacho hapo
awali takwimu zilikuwa hazioneshi kuwa wtotot hao wapo katika jamii.”
Alisistiza Mhe. Mwakyembe.
Aidha Waziri Mwakyembe
aliushukuru uongozi wa Mkoa wa Kagera kwa kuvuka asilimia ya kitaifa kwa
uandikishaji wa vizazi na vifo kwani kwa
Mkoa ni asilimia 12% ambapo kitaifa ni asilimia 11% na Wilaya ya Bukoba
inaongoza kwa asilimia 45%, Wilaya ya mwisho ni Kyerwa ambayo kwasasa imeandikisha
asilimia 9.4%.
Angalizo, Waziri
Mwakyembe pamoja na kuushukuru uongozi wa Mkoa na kumuomba Mkuu wa Mkoa na Wakuu wa Wilaya kuongeza
juhudi za uhamasishaji wa wananchi kuona umuhimu wa kuandikisha watoto wao
lakini alitoa angalizo kuwa Mkoa lazima kuwa makini sana katika uandikishaji
huo ili kudhibiti wahamiaji toka nje ya nchi kuandikishwa .
Tatu, Waziri Mwakyembe
alisema amekuja Mkoani Kagera kuona tatizo la mlundikano wa Wafungwa na mahabusu Magerezani ambapo alisema kuwa amekuwa
akitembelea Magereza kila Mkoa alipofanya ziara ili kuona ukubwa wa tatizo ni
kiasi gani na kuona jinsi ya kutatua changamoto hiyo Wizara yake ikishirikiana
na Wizara ya Mambo ya Ndani.
Waziri Mwakyembe
alisema kuwa badala ya kuongea na raia juu ya tatizo la mlundikano wa wafungwa
yeye akishirikiana na Waziri wa Mambo ya Ndani waliamua waongee na wafungwa ili
kujua tatizo kwa undani na katika kuongea na wafungwa hao katika Magereza
mbalimbali nchini waligundua yafuatayo:-
Ucheleweshwaji wa
nakala za hukumu za kesi, jamabo ambalo
tayari Mahakama tayari zimeanza
kulishughulikia kwa kasi kubwa, pili Kesi za watuhumiwa kukaa muda mrefu bila
kusikilizwa, nalo pia mahakama imeanza kulishughulikia, na Tatu Watuhumiwa
kubambikiziwa kesi tofauti na kesi zilizowapeleka Magereza. Waziri Mwakembe
alisema matatzo yote hayo sasa yanashughulikiwa kwa kasi kubwa sana na Mahakama.
Aidha, katika hatua
nyingine Mhe. Mwakyembe alitembelea Ofisi ya Wakala wa Usajili Ufilisi na
Udhamini (RITA) katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Bukoba na kumuagiza Kaimu
Mtendaji Mkuu kuhaikikisha anaiwezesha ofisi hiyo vifaa vya kisasa kama
(Kompyuta) ili kurahisisha utendaji kazi kwani Wilaya hiyo imepiga hatua kubwa
katika uandikishaji, vile vile aligawa vyeti vya kuzaliwa kwa wanaume watano na
wanawake watano.
Waziri Mwakyembe
atakuwepo Mkoani Kagera kwa siku tatu tarehe 14-16/07/2016 na anatarajia
kutembelea Mahakama kuu, Gereza la Mkoa
Bukoba, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Gereza la Wilaya ya Muleba
na Gereza la Wilaya ya Biharamulo na kuhitimisha ziara yake Wilayani humo.
|
No comments:
Post a Comment