TAKWIMU BORA ZA HATUA
YA MAKUDI EURO 2016.
Hatua ya makundi ikiwa inaanza
Jumamosi hii na Jumapili , na timu zilizofuzu kwenda hatua ya mtoano zikiwa
zishajulikana hebu tutizame takwimu bora zaidi zilizojitokeza katika hatua ya
makundi Euro 2016.
- Magoli 49 chini ya 69
yaliyofungwa Euro 2016 yamefungwa kipindi cha pili 27.5% yamefungwa dakika
ya 80 kuendelea na magoli mengi zaidi (3) yamefungwa dakika ya 92 ya
mchezo kushinda dakika kumi za mwanzo.
- Timu ya Ufaransa imeongoza kwa
jumla ya dakika 17 pekee katika mechi zao tatu Euro 2016.
- Wachezaji 12 wa timu ya
Liverpool na wachezaji 12 wa timu ya Juventus wanaoshiriki Euro 2016 wote
wamefanikiwa kufuzu kwenda hatua ya mtoano na timu zao.
- Italy na Spain zitakutana kwa
mara ya nne mfululizo katika Euro 3 pale zitakapo cheza kwenye mechi yao
ya hatua ya mtoano.
- Cristiano Ronaldo aliweza kuweka
rekodi ya kucheza mechi nyingi zaidi kwenye michuano ya Euro (17)
alipocheza dhidi ya timu ya Hungary kwenye mechi ya mwisho ya hatua ya
makundi.
- Timu 9 kati ya 24 zimemaliza
hatua ya makundi bia kufungwa 3 ya hizo zimetokea Group F.
- Kevin De Bruyne (17), Dimitri
Payet (14) na Mesut Ozil (12) ndiye wachezaji waliongoza kwa kutengeneza
nafasi za magoli.
- Kutokana na mpangilio wa mechi
hatua ya mtoano fainali ya Euro 2016 ina hakika ya kuchezwa na angalau
timu moja ambayo haijawahi kushinda kombe hili.
- Wachezaji wa timu ya Iceland
walishangilia na asilimia 8 ya wananchi wake wote walipofunga goli dhidi
ya Austria liliowapa ushindi na kuwapeleka kwenye hatua ya mtoano.
- Asilimia 50 ya matokeo ya
ushindi ya timu wa timu ya Ireland kwenye michuano mikubwa iliowahi
kushiriki ni matokeo ya ushindi wa 1-0 dhidi ya timu ya Italy.
- Cristiano Ronaldo amekuwa
mchezaji wa kwanza kufunga kwenye michuano ya Euro minne tofauti.
- Kipa wa timu ya Hungary Gabor
Kiraly, 40, ndye mchezaji mzee zaidi kuwahi kushiriki michuano ya Euro.
- Kichapo cha 2-1 dhidi ya Croatia
ni kichapo cha pili tu ambacho mchezaji Alvaro Morata amewahi kupokea
kwenye mechi ambayo amefunga baada ya kile cha 2-1 dhidi ya Barcelona
kwenye fainali ya ligi ya mabingwa.
- Spain wamekosa penati zao 4 kati
ya 7 za mwisho walizopiga kwenye michuano ya Euro.
- Petr Cech kafungwa magoli 20
kwenye michuano ya Euro zaidi ya mchezaji mwingine yeyote kasoro Peter
Schmeichel aliyefungwa 21.
- Portugal ndiye timu pekee ambayo
imefuzu kwenda hatua ya mtoano bila kushinda mechi hata moja.
- Zlatan Ibrahimovic alipiga shuti
moja tu katika mechi zake tatu Euro 2016.
- Katika mechi kati ya Ujerumani
na Northern Ireland Toni Kroos alifikisha pasi nyingi zaidi (111) kushinda
timu nzima ya Northern Ireland(105).
- Belgium walipiga pasi 28 kabla
ya kufunga goli lao dhidi ya Ireland, hii ni idadi kubwa zaidi ya Pasi
zilizozalisha goli tangia Euro 1980.
- Kwenye mechi dhidi ya timu ya
Portugal Iceland iliweka rekodi ya michuano ya Euro ya kuwa timu yenye
‘possession’ ndogo zaidi (27.8%) bila kufungwa mechi.
- Kichapo dhidi ya Croatia
kilikuwa kichapo cha kwanza cha timu ya Spain kwenye mechi ya Euro ambayo
waliongoza.
|
No comments:
Post a Comment