Pichani ni Mradi wa maji wenye
thamani ya shilingi milioni 81 mjini Katesh wilayani Hanang uliofadhiliwa na
kampuni ya bia ya serengeti ikiwa ni mkakati wa kuwapatia wakazi wa eneo hilo
maji safi na salama.
Juni 22, 2016- Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) imezindua mradi wa
maji wenye thamani ya shilingi milioni 81 mjini Katesh wilayani
Hanang’ ikiwa ni mkakati wa kuwapatia wakazi wa eneo hilo maji safi na salama.
Mradi huo wenye uwezo wa kuwahudumia
watu 12,000 unajumuisha kisima kilichochimbwa pamoja na mifumo yake, pampu ya
maji inayotumia nishati ya jua na tenki la maji ukiwa na uwezo wa
kuzalisha lita 45,000 za maji kila baada ya saa sita.
Akizungumza latika hafla ya uzinduzi
huo, Mkurugenzi wa Mahusiano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti John
Wanyancha, alisema kuwa kisima hicho ni mkakati wa kampuni hiyo ya
bia wa kuisaidia jamii chini ya mpango uitwao Maji ya Maisha na kuongeza kuwa
SBL imeshatekeleza miradi kama hiyo katika mikoa
ya Iringa, Kilimanjaro, Mwanza, Tanga, Ruvuma, Dar es Salaam,
Pwani na Dodoma ambayo imenufaisha watu zaidi ya milioni moja kwa
kuwapatia maji safi na salama.
Wanyancha alisema kuwa mradi wa
Katesh sio tu kwamba utaboresha afya za wenyeji wa eneo husika bali
pia utaongeza uzalishaji kiuchumi “hususani miongoni mwa wanawake na
watoto wa kike ambao hawatalazimika kutumia saa nyingi
kutafuta maji sehemu nyingine. Hii inatoa fursa kwa watoto wa kike kuhudhuria
masomo shuleni.”KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
|
Friday, June 24, 2016
Home
MATUKIO
MAFANIKIO YETU:-Kampuni ya Bia Serengeti yazindua mradi wa maji wa 81m/- Katesh, Hanang.
MAFANIKIO YETU:-Kampuni ya Bia Serengeti yazindua mradi wa maji wa 81m/- Katesh, Hanang.
Tags
# MATUKIO
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
MATUKIO
Labels:
MATUKIO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment