AJALI/PICHA:-Watu watatu raia wa Rwanda wafariki Dunia baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupata ajali kisha kuteketea kwa moto wilayani Ngara mkoani Kagera. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, June 24, 2016

AJALI/PICHA:-Watu watatu raia wa Rwanda wafariki Dunia baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupata ajali kisha kuteketea kwa moto wilayani Ngara mkoani Kagera.

Watu watatu raia wa Rwanda wamefariki Dunia baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupata ajali kisha kuteketea kwa moto katika kijiji cha Mshikamano Kilichopo Kata ya Rusumo wilayani Ngara mkoani Kagera.

Kaimu Mkuu wa Jeshi la Polisi wilayani Ngara mkoani Kagera Bw.Mohamed Kipano amewataja marehemu hao kuwa ni Hategekaimana Theophil (30) ambae alikuwa Dereva na Bizimana Shaabani (29) ambao waliteketea kwa moto huo Papo hapo na mwingine Alafa Nduwayo (32) ambae alifariki muda mfupi baada ya kufikishwa katika Hospitali ya Nyamiaga wilayani humo akiwa majeruhi.
Ajali hiyo imelihusisha gari aina Astros Benzi lenye namba za usajiri RAB 229 V Mali ya kampuni ya MERES ya nchini Rwanda lililo kuwa na mafuta ya diesel ambalo lililo feli breack na kushindwa kumudu Mteremko wenye kona kali katika eneo la MACHINJIONI.

Katika eneo la Ajali ilipotokea,Mwenyekiti wa Kijiji cha Mshikamano, Kata ya Rusumo wilayani Ngara mkoani Kagera ,Bw. Lameck Luhenange amesema kuwa eneo hilo linajulikana kwa jina la MACHINJIONI na linaelezwa kuwa tishio kwa maisha ya madereva na abiria kwani matukio ya ajali yameanza tangu mwaka 1985.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad