KOMBE LA SHIRIKISHO, CAF:-Yanga SC yaanza vibaya mechi zake za Makund Ikifungwa na MO Bejaia 1 - 0. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, June 20, 2016

KOMBE LA SHIRIKISHO, CAF:-Yanga SC yaanza vibaya mechi zake za Makund Ikifungwa na MO Bejaia 1 - 0.

Wawakilishi wa Tanzania katika Kombe la Shirikisho la Soka Afrika ( CAF ), Yanga SC usiku wa kuamkia leo,June 20, 2016, imeanza vibaya mechi zake za makundi ya Kombe hilo baada ya kufungwa bao 1-0 na MO Bejaia huko Algeria.

Yanga watalazimika kuzikata kilomita 6120 kurejea nyumbani Tanzania kabla ya kujipanga kukutana na Kisiki kingine ,timu ya TP Mazembe ya DRC.

Bao ambalo liliimaliza Yanga SC , lilifungwa Dakika ya 20 na Salhi.

Baada ya Mechi 1 kwa kila Klabu, Yanga SC wapo Nafasi ya 3 katika Kundi A ambalo linaongozwa na TP Mazembe ya Congo DR na kufuatia Mo Bejaia na mkiani wapo Medeama ya Ghana.

Mapema, TP Mazembe iliitandika Medeama 3-1 huko Mjini Lubumbashi Nchini Congo DR.
Baada ya Mechi hizi za kwanza za Kundi A, Mechi za Pili ni hapo June 28,2016 wakati Yanga SC watakapoikaribisha TP Mazembe na Siku inayofuata Medeama wako kwao Ghana kucheza na MO Bejaia.

CAF Kombe la Shirikisho.

KUNDI A.

-MO Bejaia (Algeria)
-Yanga (Tanzania)                                                                                    
-TP Mazembe (DR Congo)
-Medeama (Ghana)

KUNDI B.

-KAC Marrakech (Morocco)
-Etoile du Sahel (Tunisia)
-FUS Rabat (Morocco)
-Ahly Tripoli (Libya)

MECHI ZA MAKUNDI -RATIBA/MATOKEO.

Juni 28,2016.

Al-Ahli Tripoli – Libya v KAC Marrakech - Morocco  
    
Yanga - Tanzania    v TP Mazembe - Congo, DR

Juni 29,2016.

ES Sahel – Tunisia v FUS de Rabat - Morocco  

Medeama – Ghana v MO Bejaia - Algeria

Mechi za 3.

Julai 15,2016.

KAC Marrakech – Morocco v FUS de Rabat - Morocco

Yanga - Tanzania    v Medeama - Ghana

Julai 16,2016.

ES Sahel – Tunisia v Al-Ahli Tripoli - Libya

Julai 17,2016.

MO Bejaia – Algeria v TP Mazembe - Congo, DR        

Mechi za 4.

Julai 26,2016.

Al-Ahli Tripoli – Libya v ES Sahel - Tunisia   
     
Medeama – Ghana v Yanga – Tanzania

Julai 27, 2016.

FUS de Rabat – Morocco v KAC Marrakech - Morocco

TP Mazembe - Congo, DR v MO Bejaia - Algeria

Mechi za 5.

Agosti 12, 2016.

Al-Ahli Tripoli – Libya v FUS de Rabat - Morocco  
      
Agosti 13, 2016.

ES Sahel – Tunisia v KAC Marrakech - Morocco

Yanga – Tanzania v MO Bejaia – Algeria

Agosti 14, 2016.

Medeama – Ghana v TP Mazembe - Congo, DR

Mechi za 6.

Agosti 23, 2016.

KAC Marrakech – Morocco v Al-Ahli Tripoli - Libya    
  
FUS de Rabat – Morocco v ES Sahel - Tunisia   

TP Mazembe - Congo, DR v Yanga - Tanzania  

MO Bejaia – Algeria v Medeama - Ghana

NUSU FAINALI.

**Mechi za Kwanza Septemba 16-18, 2016 na Marudiano Septemba 23-25, 2016.

Mshindi wa 2 Kundi B v Mshindi Kundi A

Mshindi wa 2 Kundi B v Mshindi Kundi A

FAINALI.

Mechi ya Kwanza Oktoba 28-30, 2016 na Marudiano Novemba 4-6, 2016

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad