Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama
Cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye amenena tena kuhusu uamuzi wa waziri mkuu wa
zamani, Edward Lowassa kukihama chama hicho na kujiunga na Chama Cha Demokrasia
na Maendeleo (CHADEMA) na kupewa nafasi ya kugombea urais.
Nape ameeleza kuwa uamuzi huo
uliwasaidia kwa kiasi kikubwa kwani mwanasiasa huyo aliyekuwa na nguvu kubwa
ndani ya chama hicho alikuwa alama ya ufisadi kutokana na kukabiliwa na tuhuma
nyingi za ufisadi.
“Lowassa
alikuwa alama ya ufisadi, alipoondoka aliturahisishia kazi. Watu walikuwa
wanahusisha ufisadi na umasikini, walichoka na walikuwa radhi kuchagua hata
jiwe lakini sio CCM,” alisema Nape.
Alisema kuwa angepata nafasi ya
kumshauri Lowassa katika siasa, angemshauri ajiuzulu siasa kabla hajaondolewa
kwa aibu katika medani za siasa.
Kadhalika, Nape alisema kuwa kosa
kubwa ambalo lilifanywa na vyama vya upinzani ni kumpokea Lowassa ambaye amedai
alikuwa amesababisha CCM kupakwa matope ya uchafu kutokana na kuwa na tuhuma
nyingi.
Hata hivyo, Nape alimpongeza Lowassa
kwa kukubali matokeo ya uchaguzi mkuu kwa kuwa uamuzi huo ulisaidia kuliweka
Taifa katika hali ya amani baada ya uchaguzi.
Lowassa amekuwa akikanusha tuhuma
zote zilizokuwa zikielekezwa kwake hususan tuhuma za kuhusika na sakata la
Richmond lililosababisha ajiuzulu nafasi ya Uwaziri Mkuu katika Serikali ya
Awamu ya Nne.
Alijiunga na CHADEMA na kugombea
nafasi ya URAIS akiungwa mkono na vyama vya siasa vinavyounda UKAWA.
Alipata kura takribani milioni 6 na
kusaidia kupata wabunge wengi zaidi wa upinzani akiweka historia ya ushindani
mkubwa zaidi kuwahi kutokea kwenye uchaguzi mkuu tangu kuanzishwa kwa mfumo wa
vyama vingi nchini.....SOMA ZAIDI KWA KUBOFYA HAPA.
|
Monday, June 20, 2016
NAPE NNAUYE:-..Asema Lowassa ni Alama ya Ufisadi.
Tags
# SIASA
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
SIASA
Labels:
SIASA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment