Mpambano wa Kundi
F la EURO 2016 uliochezwa Jana,June 18, 2016 huko Nchini Ufaransa zilimalizika
kwa matokeo ya Sare.
Huko Stade
Velodrome, Marseilles, Iceland na Hungary zilitoka sare ya bao 1-1 na Mabao
kufungwa Dakika ya 40 kwa Penati ya upande wa Iceland iliyopigwa na Gylfi
Sigurdsson na Hungary kusawazisha Dakika ya 88 kwa Bao la kujifunga mwenyewe la
Birkir Mar Saevarsson.
Huko Parc
des Princes, Paris, Ureno na Austria zilitoka Sare ya 0-0 na Cristiano Ronaldo
kuikosesha Ureno Bao katika Dakika ya 79 alipokosa Penati.
Matokeo hayo
yameziacha Timu zote 4 za Kundi F zilizobakisha Mechi 1 kuwa na nafasi za
kusonga Raundi ya Mtoano ya Timu 16.
Kwenye Kundi
F, Hungary wanaongoza wakiwa na Pointi 4 kisha ni Ureno na Iceland wenye Pointi
2 kila mmoja na wa mwisho ni Austria wenye Pointi 1.
EURO 2016
– RATIBA /MATOKEO.
**Saa za
Bongo.
Jumamosi
Juni 18,2016.
KUNDI E, Belgium 3 - 0 Republic of Ireland
KUNDI F, Iceland 1 – 1 Hungary
KUNDI F, Portugal 0 – 0 Austria
Jumapili
Juni 19,2016.
KUNDI A, Romania v Albania (2200, Stade
de Lyon)
KUNDI A, Switzerland v France (2200, Stade
Pierre Mauroy, Lille)
Jumatatu
Juni 20,2016.
KUNDI B, Russia v Wales (2200, Stadium
de Toulouse)
KUNDI B, Slovakia v England (2200, Stade
Geoffroy Guichard)
Jumanne
Juni 21,2016.
KUNDI C, Ukraine v Poland (1900, Stade
Velodrome)
KUNDI C, Northern Ireland v Germany
(1900, Parc des Princes)
KUNDI D, Czech Republic v Turkey (2200,
Stade Bollaert-Delelis)
KUNDI D, Croatia v Spain (2200, Stade de
Bordeaux)
TIMU
ZILIZOFU KUINGIA RAUNDI YA MTOANO YA TIMU 16.
-KUNDI A:
Ufaransa
-KUNDI D:
Hispania
-KUNDI E:
Italia
**Bado
Timu 14
**Washindi
Wawili wa juu wa Kila Kundi na Timu Bora 4 zilizomaliza Nafasi za Tatu
zitaingia Raundi ya Mtoano ya Timu 16.
|
No comments:
Post a Comment