COPA AMERICA 2016 -RATIBA/MATOKEO:-Argentina na Chile zenda Nusu Fainali zikishinda 4-1 na 7-0. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, June 19, 2016

COPA AMERICA 2016 -RATIBA/MATOKEO:-Argentina na Chile zenda Nusu Fainali zikishinda 4-1 na 7-0.

Mabingwa Watetezi wa Copa America, Chile Leo,June 18, 2016 wameenda hatua ya  Nusu Fainali ya Mashindano hayo ya Copa América Centenario 2016 kwa kishindo kwa kuicharaza Mexico magoli 7 - 0 kwenye dimba la Levis Stadium,Santa Clara Califonia.

Bao za Chile, ambao waliongoza 2-0 hadi mapumziko , zilifungwa na Eduardo Vargas aliyefunga mara 4, dakika ya 15, 51, 56 na 73 Huku Edson Puch akifunga goli 2, dakika ya 44 na 86, naye Alexis Sanchez akifunga goli moja dakika ya 48. 
Nao Argentina wametinga Nusu Fainali ya Mashindano ya Copa América Centenario kwa kuicharaza Venezuela goli 4 - 1 huko Gillette Stadium, Foxborough, Massachusetts.

Bao za Argentina zilifungwa na Gonzalo Higuain, Dakika ya 8 na 28, Lionel Messi, Dakika ya 60 na Erik Lamela Dakika ya 71 wakati lile la Venezuela lilifungwa Dakika ya 70 na Salomon Rondon.

Messi alianza Mechi hii ikiwa ni mara yake ya kwanza kuanza Mechi katika Mashindano haya na kuikuta rekodi ya Lejendari wa Argentina, Gabriel Batistuta, ya kuifungia Argentina Bao 54 ikiwa ni Rekodi ya Ufungaji Bora kwa Nchi hiyo.

Kwenye Nusu Fainali, Argentina watacheza na Wenyeji Marekani-USA wakati Nusu Fainali nyingine Colombia dhidi ya Chile.

COPA AMERICA 2016 -RATIBA/MATOKEO.

**Saa za Bongo

NUSU FAINALI

Jumatano 22 Juni 2016.

0400 USA v Argentina

Alhamisi 23 Juni 2016.

0300 Colombia v Chile   
  
MSHINDI WA TATU.

Jumapili 26 Juni 2016

0200

FAINALI.

Jumatatu 27 Juni 2016.

0300 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad