EURO 2016:- Mabingwa Hispania watinga Mtoano. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, June 18, 2016

EURO 2016:- Mabingwa Hispania watinga Mtoano.

Mabingwa Watetezi,Hispania wametinga Raundi ya Mtoano ya Timu 16 kwa kishindo huku wakiwa na Mechi 1 mkononi baada ya Jana Usiku ,June 17, 2016  kuichapa Uturuki 3-0 huko Stade de Nice, Nice, Nchini Ufaransa katika Mechi ya Kundi D la la EURO 2016.

Bao la Kichwa cha Alvaro Morata dakika ya 34’’alieunganisha Krosi ya Nolito na Nolito kupiga Bao la Pili dakika ya 37’’ huku Bao lao la 3 likifungwa na Alvaro Morata dakika ya 48’’.
Matokeo hayo yanaufanya Msimamo Kundi D baada ya Mechi mbili kwa kila Timu, Hispania kuongoza kundi kwa Pointi 6, wakifuatiwa na Croatia na Pointi 4, Czech Republic Pointi 1 na mkiani ni Uturuki wenye Pointi 0.

TIMU ZILIZOFU KUINGIA RAUNDI YA MTOANO YA TIMU 16.

-KUNDI A: Ufaransa

-KUNDI D: Hispania

-KUNDI E: Italia

**Bado Timu 14

**Washindi Wawili wa juu wa Kila Kundi na Timu Bora 4 zilizomaliza Nafasi za Tatu zitaingia Raundi ya Mtoano ya Timu 16.
Leo, Jmamosi June 18, 2016, zipo Mechi 3 ambapo KUNDI E itakuwa ni Belgium v Republic of Ireland huko Stade de Bordeaux Mjini Bordeaux wakati huko Stade Velodrome, Marseille ipo Mechi ya KUNDI F Iceland v Hungary na nyingine ya KUNDI F ni Portugal v Austria itakayochezwa Parc des Princes, Paris.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad