Waziri wa Fedha na Mipango wa Tanzania, Dk Philip
Mpango ,Jumatano ,June 01,2016, alibanwa bungeni baada ya wabunge kutaka maelezo ya kina ya sababu
za Serikali kushindwa kuwasilisha muswada wa kurekebisha Sheria ya Manunuzi
ambao unalalamikiwa kuwa unachochea ufisadi.
Sheria hiyo imekuwa ikilalamikiwa na
wadau, wakiongozwa na Rais John Magufuli, kuwa inatoa mwanya kwa wazabuni
kupandisha bei za bidhaa wanapopewa mikataba ya Serikali kwa kushirikiana na
watumishi wa umma.
Rais Magufuli alilalamikia sheria
hiyo kwa mara ya kwanza Novemba mwaka jana wakati akizindua Bunge, akisema
inaumiza Serikali na hivyo itafanyiwa marekebisho.
Juzi, wabunge wa CCM walisimama
kidete wakimtaka waziri huyo kuwa na majibu yanayoridhisha na kueleza kuwa
asipofanya hivyo, wangekwamisha bajeti yake, ambayo hata hivyo ilipita.
Akichangia hotuba ya Wizara ya Fedha,
Mashimba Ndaki alisema Sheria ya Manunuzi imekuwa ikisababisha kero kubwa kwa
wananchi na kuwasababishia usumbufu usiokuwa na maana.
Ndaki alisema sheria hiyo haifai,
lakini inashangaza kuona Serikali imekuwa kimya. Janeth Mbene alisema
haiwezekani kuendelea kufumbia macho jambo hilo tena.
Mbene alisema pamoja na udhaifu wa
sheria hiyo, Serikali inatakiwa kuangalia upya kwa kuwa yako mashirika mengi
ambayo ni mzigo hivyo akaomba yaondolewe na kufutwa.
Mbunge wa Mpwapwa, George Lubeleje
alisema sheria ya manunuzi ni mchwa unaotafuna kila mali za umma, lakini
Serikali inaonekana kufumbia macho.
"Mimi
nimekuwa mjumbe wa bodi ya mashirika mbalimbali, lakini utakuta vitu
vinavyonunuliwa na watu moja kwa moja, bei inakuwa chini lakini kwa kupitia bei
ya Sheria ya Manunuzi inauwa mara mbili yake, huu ni wizi,” alisema Lubeleje.
Mbunge wa viti maalumu (CCM), Ritha
Kabati alisema sheria hiyo imekuwa ikiwanyima nafasi wazalendo.
|
No comments:
Post a Comment