TAZAMA PICHA / VIDEO COPA AMERICA 2016:-Messi ajiuzulu baada ya kukosa penati..Chile ikiibuka Bingwa. - Mwana Wa Makonda
cV7ufzj

Muhtasari

X-BET

MAIN-

Post Top Ad

cV7ufzj

Monday, June 27, 2016

demo-image

TAZAMA PICHA / VIDEO COPA AMERICA 2016:-Messi ajiuzulu baada ya kukosa penati..Chile ikiibuka Bingwa.

.com/simgad/
Chile-win-the-Copa-America-Centenario-final
Mshambulizi wa Argentina na FC Barcelona ya Hispania, Lionel Messi amestaafu kutoka soka ya Kimataifa.

Mchezaji huyo bora zaidi duniani alitangaza hatua hiyo baada ya kukosa penalti iliyoiwezesha Chile kuilaza Argentina katika fainali ya mchuano wa Copa America 2016.

"Kwangu mimi ,soka ya kimataifa ama hata kuichezea Argentina sitaweza tena.

''Nimefanya kila niwezalo.''

''Kwa kweli inaniumiza kuwa sijawahi kutwaa kombe lolote la kimataifa'' alisema mshambulizi huyo mwenye umri wa mia 29.

Mshambulizi huyo ameisaidia Mabingwa wa ligi kuu ya Uhispania Barcelona, kutwaa mataji 8 na mataji manne ya ubingwa wa bara ulaya.

Hata hivyo kimataifa Messi amewahi kushinda taji moja tu lile la nishani ya dhahabu ya Olimipiki ya mwaka wa 2008 Olympic.
Copa-America-Final-Penalty-shootout
Argentina imeshindwa katika fainali tatu za kimataifa.

Argentina walilazwa moja kwa nunge na Ujerumani katika kombe la dunia la mwaka wa 2014 huko Brazil.

Timu hiyo aidha imeshindwa na Chile mara mbili katika fainali za mchuano wa Copa America kupitia kwa mikwaju ya penalti.

Messi vilevile alikuwa katika kikosi kilichoshindwa na Brazil katika mchuano huo wa mwaka wa 2007 wa Copa America.

Argentina walitoka sare ya 0-0 baada ya muda wa kawaida na ule wa ziada wa dakika 120.

Akiwa Uhispania Messi ametikisa wavu mara 453 kati ya mechi 531 alizoshiriki.

Aidha Messi ndiye anayeshikilia rekodi ya mfungaji bora wa La Liga akiwa na mabao 312.
Maskini-Messi-1
Kipa wa Chile, Claudio Bravo akiinua Kombe la Copa America Centenario baada ya kulitwaa usiku wa kuamkia leo kwa kuifunga Argentina kwa penati 4-2 kufuatia sare ya 0-0 ndani ya dakika 120 Uwanja wa MetLife, East Rutherford mjini New Jersey, Marekani.
1
Mwanasoka bora wa dunia, Lionel Messi alikosa penati ya kwanza ya Argentina sawa na Lucas Biglia aliyekosa ya nne.
2
Waliofunga penalti za Argentina ni Javier Mascherano na Sergio Aguero wakati za Chile zilifungwa na N. Castillo, C. Aránguiz, J. BeausejourF. Silva huku  A. Vidal akikosa ya kwanza tenaHata hivyo Chile waliibuka videdea kwa mabao 4-2 kupitia mikwaju ya penati.
4

6

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Contact Form

Name

Email *

Message *