Cristiano
Ronaldo akaenda kwa kujiamini kupiga penalti ya mwisho ya Real Madrid na
kumtungua kipa Jan Oblak wa Atletico Madrid kuwapa Magalactiico taji la 11 la Ligi ya
Mabingwa.
Wengine waliofungaa penalti za Real Madrid ni Lucas Vazquez, Marcelo, Gareth Bale na Sergio Ramos, wakati Atletico zimefungwa na Antonio. Griezmann, Gabi na Saul. |
Kipa Keilor
Navas Gamboa alijitanua vizuri langoni na Juan Francisco Torres Belen
‘Juanfarn’ akaona lango dogo na kugongesha nguzo ya pembeni penalti ya nne ya
Atletico Madrid.
|
Mchezo huo uliochezeshwa na marefa wa
Uingereza, Mark Clattenburg aliyesaidiwa na Simon Beck na Jake Collin, Real
Madrid walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa beki wake na Nahodha, Sergio
Ramos dakika ya 15 aliyemalizia mpira wa kichwa wa winga Gareth Bale.
Kipindi cha pili, kocha Diego Simeone wa Atletico alianza na mabadiliko, akimpumzisha kiungo Muargentina mwenzake Augusto Matias Fernandez na kumuingiza kiungo Mbelgiji Yannick Ferreira Carrasco. Mabadiliko hayo yalikuwa msaada kwa kikosi cha Simeone, kwani ni Carrasco aliyekwenda kuisawazishia Atletico dakika ya 79, akimalizia pasi ya Juan Francisco Torres Belen, maarufu kama Juanfran. Bao hilo ‘likauamsha’ upya mchezo huo, timu zote zikicheza ka nguvu na kasi kusaka bao la ushindi, lakini dakika 90 zikamalizika kwa sare ya 1-1. |
No comments:
Post a Comment