Wakazi wa Kata ya Karansi, Wilaya ya
Siha mkoani Kilimanjaro wametoa uamuzi kuwa wanawake watakaovaa sketi fupi na
vijana watakaovalia suruali chini ya kiuno, wataadhibiwa kwa kuchapwa viboko 60
hadi 70.
Uamuzi huo umefikiwa na wakazi zaidi
ya 200 wakisema uvaaji huo ni kinyume na mila na desturi za Kiafrika.
Vazi lingine lisilotakiwa kwa
wanawake ni kuvaa suruali pamoja na vijana kunyoa ndevu mitindo isiyofaa.
Mkutano huo ulioandaliwa na wazee wa
kimila jamii ya Meru (Wachili) na Wamasai (Malaigwani), uliwavutia wananchi
wengi ambao walihudhuria.
Sambamba na uamuzi huo utakaokuwa
unafanyika hadharani, pia adhabu hiyo itawahusu wezi wa mali na wanaopenda
kucheza pool table wakati wa kazi.
Kamanda wa Polisi mkoani hapa,
Wilbrod Mutafungwa alipinga uamuzi huo akisema kwa maazimio hayo ya kuwaadhibu
watuhumiwa kwa kuwachapa viboko ni kujichukulia sheria mkononi na ni kinyume na
sheria.TAARIFA ZAIDI ..BOFYA HAPA.
|
Sunday, May 15, 2016
MAADILI YETU:-Vijana Wanaovaa Suruali Chini ya Kiuno Kuchapwa Viboko 70.
Tags
# HABARI
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
HABARI
Labels:
HABARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment