Ndanda FC ndiyo waliotangulia kupata bao
kwa penalti dakika ya 29, mfungaji Omary Mponda aliyemchambua vizuri kipa wa
Yanga SC, Deo Munishi ‘Dida’ baada ya beki Juma Abdul kumuangusha mshambuliaji
Atupele Green kwenye boksi.
Yanga SC walisawazisha bao hilo
dakika ya 36 kupitia kwa mfungaji bora wa Ligi Kuu msimu uliopita, Simon Msuva
kwa shuti kali akimalizia krosi ya winga Geoffrey Mwashiuya.
Mshambuliaji hatari kutoka Zimbabwe,
Donald Ngoma akaifungia Yanga SC bao la pili dakika ya 41 kwa shuti kali pia akimalizia
krosi ya beki wa kushoto, Mwinyi Hajji Mngwali.
|
Kipindi cha
pili, timu zote zilianza na mabadiliko, Yanga SC wakimpumzisha Mwinyi Mngwali na
kumuingiza Oscar Joshua na Ndanda wakimpumzisha Riffat Hamisi na kuingia Ahmed
Msumi.
Mabadiliko
hayo yaliinufaisha Ndanda FC iliyopata bao la kusawazisha dakika ya 79
lililofungwa na Minely aliyemalizia pasi ya Atupele Green.
|
Waziri wa Kilimo na Mifugo Mhe. Mwigulu Nchemba ambaye alikuwa
mgeni rasmi wa mchezo huo alilikabidhi kombe hilo kwa nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’ baada ya
kumalizika kwa mchezo kati ya Ndanda FC dhidi ya Yanga SC na Ubingwa huo unawafanya Azam FC kulikosa taji hilo ndani ya
misimu miwili mfululizon wakati Simba SC
wao wameendelea kulikosa taji hilo ndani ya misimu minne mfululizo.
|
No comments:
Post a Comment