HARAKATI ZA SIASA TANZANIA:-Waziri Mkuu Mstaafu ,Mhe.Frederick Sumaye Ateuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu Ya CHADEMA. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, May 13, 2016

HARAKATI ZA SIASA TANZANIA:-Waziri Mkuu Mstaafu ,Mhe.Frederick Sumaye Ateuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu Ya CHADEMA.

Waziri Mkuu Mstaafu,Mhe.Fredrick Sumaye ameteuliwa kuwa mjumbe wa Kamati Kuu (CC) ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Mwenyekiti wa CHADEMA – Taifa,Mhe. Freeman Mbowe,amekiambia Kikao cha Kamati Kuu Jana,May 12, 2016, kuwa, anampendekeza Sumaye kuwa mjumbe wa CC kwa lengo la kuimarisha chama hicho.

Amesema, dhamira ya CHADEMA ni kujiimarisha kwa ajili ya uchaguzi ujao, kwa kutumia kila Mwanachama kufanya kazi ya uenezi.

Kamati Kuu imeridhia uteuzi wa Mhe.Sumaye kuwa mjumbe wa Kamati Kuu.

Kwa Upande wake,Mhe. Sumaye amemshukuru Mbowe kwa kumteuwa kushika nafasi hiyo na kuahidi kukitumikia chama hicho kwa nguvu zake zote.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad