Mikoa ya Iringa,
Kilimanjaro, Kagera na Morogoro ndiyo inayotajwa kuwa na idadi kubwa ya watoto
wanaosafirishwa nje ya nchi kwa ajili ya kutumikishwa, utumwa pia dhamana ya
deni.
Hata hivyo, juhudi
kubwa zinapaswa kuchukuliwa ili kulinda watoto dhidi ya unyanyasaji, ubakaji,
ukahaba, kazi za kulazimishwa, utumwa na dhamana ya deni.
Akizungumza na
MwanaHALISI Online ,May 17,2016, kwa njia ya simu Angel Benedicto, Mwanzilishi na
Mkurugenzi Mtendeji wa Shirika la Wote Sawa lenye ofisi zake jijini Mwanza
ambalo linatete wafanyakazi wa majumbani amesema “licha ya uwepo wa sheria ya
kuzuia usafirishaji haramu wa binadamu ya mwaka 2008, bado tuna kazi kubwa
kuzuia usafirishaji wa watoto.”
Amesema, ukubwa wa
tatizo hili unatokana na umasikini katika familia nyingi, baadhi ya watendaji
wa taasisi za serikali wakiwemo askari wa Jeshi la Polisi, maofisa watendaji na
viongozi wa serikali za vijiji na kata kukosa uelewa kuhusu dhana ya
usafirishai binadamu wakiwemo watoto.
“Hili ni tatizo kubwa.
Pia jamii haina uelewa wa kutosha kuhusu tatizo hili, mwingine anaweza kutenda
kosa bila kujua.
“Tunapofungua kesi
nyingi zinaishia polisi. Kwa kuwa polisi nao wakati mwingine hawaelewi dhana
nzima ya usafirishaji haramu wa binadamu,” amesema Angel.
Amesema, watoto wenye
umri wa miaka 14 hadi 16 ndio wanaoongoza kwa kusafirishwa wakifuatiwa na wale
wenye umri wa miaka saba hadi 10.
Mikoa inayoongoza kwa usafirishaji ni Iringa
(asilimia 15), Kilimanjaro (asilimia 9), Kagera (asilimia 9), Morogoro (asilimia
9), Dodoma (asilimia 7), Kigoma (asilimia 7) na Mbeya (asilimia 7).
“Katika kuhakikisha
tunaondoa tatizo hili, tayari Wote Sawa tuna mradi wa kutoa elimu kwa mahakimu,
wanasheria, wakuu wa wilaya, watendaji wa kata na wenyeviti wa vijiji katika
mikoa 10 ya Ruvuma, Tabora, Mtwara, Arusha, Mwanza, Iringa, Mbeya, Dodoma, Dar
es salaam na Kigoma,” amesema.
|
No comments:
Post a Comment