CAF KOMBE LA SHIRIKISHO:-TP Mazembe yasonga Mbele...Yanga SC leo May 18,2016 na Sagrada Esperanca. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, May 18, 2016

CAF KOMBE LA SHIRIKISHO:-TP Mazembe yasonga Mbele...Yanga SC leo May 18,2016 na Sagrada Esperanca.

TP Mazembe wameendelea mbele katika michuano ya CAF ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika baada ya kupata goli la ugenini dhidi ya Stade Gabesien.

Ilikuwa baada ya matokeo ya mchezo wa mwisho kuisha kwa jumla ya magoli 2-2.

TP Mazembe, Mabingwa wa Afrika,waliingia katika mchezo wa pili siku ya Jana Jumanne,May 17,2016 huku wakiwa nyuma kwa 2-1 mjini Gabes kutokea kwenye mchezo wake wa kwanza na ushindi wa goli 1-0 ukaifanya kusonga mbele.

TP Mazembe waliingia katika michuano hii baada ya kutolewa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Wydad Casablanca ya Morocco. 

Michezo mingine inapigwa leo hii,Jumatano May 18,2016, ambapo Mabingwa wa Tanzania Yanga SC watakuwa ugenini kwa faida ya magoli 2 -0 ya nyumbani kukipiga dhidi ya Sagrada Esperanca, wakati Timu ya Mounana watacheza na Etoile du Sahel huku Medeama wakipepetana na Mamelodi Sundowns ya Afrika kusini.

Misr Elmaqasah kutoka Misri watacheza na Al Ahly Tripoli ya Libya huku Kawkab Marrakech wakiwakaribisha Al Merreikh na baadaye FUS Rabat ya Morocco wakikipiga dhidi ya Stade Malien kutoka Mali.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad