MATOKEO/RATIBA EPL 2015 / 2016:- Man United waenda Ligi ya Europa. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, May 18, 2016

MATOKEO/RATIBA EPL 2015 / 2016:- Man United waenda Ligi ya Europa.

Kipa David de Gea akanyimwa tuzo ya "Glavu za Dhahabu' baada ya kutunguliwa na beki wake, Chris Smalling aliyejifunga dakika ya mwisho.

Marcus Rashford alikuwa kivutio baada ya Manchester United kufuzu moja kwa moja kucheza michuano ya Ligi ndogo ya ulaya (Europa League 2016 / 2017) baada ya kuwachapa Bournemouth katika mchezo wao wa ligi uliokuwa wa kiporo Hapo Jana May 17,2016,usiku na kushinda mabao 3-1.

Wayne Rooney alikuwa wa kwanza kuiandikia bao la kwanza, baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Antony Martial kabla ya Marcus Rashford kupachika la pili na baadaye Ashley Young kumalizia la tatu.

Goli la tatu na la ushindi kwa Man United liliifanya timu hiyo kukaa juu ya Southampton,ambao wataingia katika michuano midogo ya ligi ya Ulaya (Europa League) lakini kwa kuanzia hatua ya makundi msimu ujao.

Kwa sasa Mashetani hao wekundu wanaamishia makali yao katika mchezo wa fainali ya FA utakaochezwa Jumamosi,May 21,2016 dhidi ya Crystal Palace kwenye dimba la Wembley.

Louis van Gaal, ambaye bado hatima yake haijajulikana ndani ya timu hiyo anataka kuiongoza Man United kupata taji lake la kwanza tokea walivyoshinda Ligi kuu ya Uingereza  mwaka 2013 chini ya Sir Alex Ferguson.
Man United sasa inafikisha pointi 66 kwa matokeo hayo, baada ya kucheza mechi 38 ikiwa katika nafasi ya tano, mbele ya Southampton yenye 63 za mechi 38 pia.


Leicester City ndiyo mabingwa wapya WA EPL 2015 / 2016 baada ya kumaliza na pointi 81 za mechi 38, wakifuatiwa na Arsenal wenye pointi 71, Tottenham Hotspur pointi 70 na Manchester City pointi 66, wakiwazidi Kwa wastani wa mabao mahasimu wao, Man United.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad