Mkuu wa Kitengo cha
Vifaa vya Mawasiliano wa tiGO, David Zacharia
(kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es
Salaam mapema jana kuhusu huduma iliyoanzishwa
na kampuni hiyo ya kutiririsha video za
YouTube bure ambayo itakuwa inapatikana
kwa wateja wote wa Tigo kuanzia saa 6.00 usiku hadi saa 12.00 alfajiri. Kulia
ni Meneja Mawailiano wa Tigo, John Wanyancha.
“Kitu pekee kinachohitajika ili kuweza
kupata data za bure katika kutiririsha
video za YouTube ni kuwa na aina ya simu itakachoweza data hizo.
Tunaamini huduma hii mpya
itaendelea kuonesha kujituma kwetu kwenye kuboresha mabadiliko kwenye maisha ya
kidijitali na kuongoza kutoa teknolojia
ya hali ya juu pamoja na ubinifu kwa wateja wetu,” alisema Zacharia.
Pamoja na utriririshaji huo watumiaji
wa YouTube pia wateja watakuwa na njia
mbadala ya kuweka video kwenye simu zao ambayo ni programu ya simu inayojulikana kama YouTube Offline inayomwezesha mtumiaji kuongeza video kwenye simu yake ili aweze
kuiangalia baadaye wakati ambapo muunganisho na itaneti unakuwa haupo au upo chini.
Kwa video ambazo pale ambapo
zinapatikana watumiaji wanaweza
kuchagua kuongeza video kwa kuzitiririsha
na kwa ajili ya kuangalia hapo baadaye
kwa kutumia kitufe cha ‘offline’.
Ikiwa imeshachukuliwa kwa njia hiyo video hiyo inaweza kuchezeshwa bila kuunganishwa na intaneti kwa muda wa
hadi saa 48, hivyo mtumiaji anaweza kuzifurahia video zake za YouTube bila hofu ya maunganisho na intaneti kuwa
yapo chini.
|
Meneja Mawasiliano wa
Tigo, John Wanyancha (kulia), akizungumza katika mkutano huo.
Zacharia aliongeza kwamba kuzifikia data bure kutakuwa
kunapatikana kwa wateja wa Tigo wa huduma ya malipo kabla bila kuwepo malipo maalum yanayohitajika kuifurahia huduma hiyo.
Upatikanaji bure wa
data za huduma ya kutiririsha video za YouTube umefanyika baada ya kampuni hiyo
ya simu kutangaza huduma nyingine ya
bure ya WhatsApps kwa wateja wake mwanzoni mwa mwaka huu ambako pia
kulitamnguliwa na kiuzinduliwa kwa
huduma ya Facebook ya Kiswahili mwaka 2014.
Tigo inayofuraha kujumuisha
majkuwaa ya video kwenye ofa hii. Kama wewe ni msambazaji wa huduma ya video unaweza
kuwasiliana nasi kupitiacustomercare@tigo.co.tz.
|
Wanahabari wakichukua
taarifa hiyo.
|
No comments:
Post a Comment