Mamlaka ya mawasiliano Tanzania
(TCRA) imesema kuwa asilimia 79 ya simu za kiganjani zilizofanyiwa utafiti kwa
kipindi cha Mwezi Desemba hadi Februari mwaka huu,2016, ziko salama na sio za
bandia ,huku asilimia 18 zikionekana zikiwa za bandia hivyo kuwataka Wananchi
kutambua kuwa simu feki zilizoko sokoni ni chache tofauti na kipindi cha nyuma.
Pia imebainika kuwa asilimia kubwa ya
nyumba zinazoungua na umeme ni kutokana na simu bandia ambazo betri zake au
vifaa vyake hushindwa kuhimili mionzi
pindi zinapokuwa zinachajiwa hivyo kusababisha mlipuko wa moto na hivyo kuleta
madhara .
Hayo yalisemwa na Meneja Uhusiano wa Mamlaka
ya mawasiliano Tanzania Bw.Innocent
Mungi alipokuwa akizungumza katika semina ya mfumo wa rajisi ya namba za utambulisho wa simu za kiganjani
iliyowashirikisha wadau na wafanyabiashara wa jijini hapa.
Alisema kuwa kutokana na elimu ambayo
wameitoa kwa wafanyabiashara wa simu
hizo ya kuhakiki kwanza kabla ya kuwauzia wananchi imepunguza uingizaji
wa simu feki na kwamba wamebaini kuwa asilimia 79 ni salama hazina matatizo ya
aina yeyote.
Alidai kuwa kufuatia uzimaji wa simu
bandia litakalofanyika juni 16 mamlaka hiyo imeweza kutoa elimu kwa
wauzaji,watumiaji ili kuhakikisha kuwa wanabini simu zao kama ni salama ili
kuweza kuepuka zoezi la kuzimiwa simu zao bila yawao kujiandaa.
“Wakati
tumeanza kubaini zoezi la kutambua simu feki tulibaini kuwa asilimia 30
zilikuwa bandia ila kutokana na elimu iliyotolewa hadi February simu bandia
zimepungua hadi kufikia asilimia 18 hii inaonyesha kuwa simu feki zilizoko
sokoni ni chache mno “aliongeza .
Aidha Bw.Innocent alitaja faida za kuzimiwa simu bandia kuwa ni pamoja na
kuongeza usalama mtandaoni kwa watumiaji wa simu ,kupunguza wizi wa simu na kupunguza matukio ya uhalifu ambayo
yamekuwa yakitumika mara nyingi kwa njia ya simu hizo pamoja na kuzuia matumizi
ya simu zisizokuwa na viwango.
Awali Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo
,Bw.Ally Simba aliwataka Wananchi
kufanya zoezi la kuhakiki simu zao kwa kufuata maelekezo sahii ili waweze
kubaini simu feki kabla ya kuzimiwa simu hizo juni 16 ,kwani wengi wa watumiaji
wa simu hawafuati malekezo ya kutambua simu bandia .
Bw.Simba aliseama kuwa ni vema wananchi wakatumia mfumo waliowekewa wa
kubaini simu zao kama ziko salama kwani
ifikapo juni simu zote bandia zitazimwa na kuwataka wafanyabiashara nao wawe
makini pindi wanaponunua mizigo yao ya bashara ili kuepuka hasara
watakazozipata wao na pia hasara watakazopata wanunuzi wa simu hizo.
|
No comments:
Post a Comment