HABARI / VIDEO:- Sikiliza Rais Magufuli Kuhusu Mafisadi Wanaolalamika Kutumbuliwa Hadharani . - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, April 22, 2016

HABARI / VIDEO:- Sikiliza Rais Magufuli Kuhusu Mafisadi Wanaolalamika Kutumbuliwa Hadharani .




Jana, akiongea na viongozi wa ngazi tofauti wa CCM katika hafla ya kuwashukuru kwa kazi waliyoonyesha wakati wa Uchaguzi Mkuu uliopita, Rais Magufuli alisema kama watu anaowatumbua hadharani pia waliiba hadharani, ni lazima watumbuliwe hadharani.

Magufuli alisema kuwa mateso waliyopata mamilioni ya Watanzania kutokana na kuibiwa, yanafanywa na hao wachache lazima nao waanze kupata mateso hayohayo.

Kwa hiyo ziko haki za binadamu kwa matajiri tu kwa hawa walioibiwa hakuna haki,” aliuliza Rais Magufuli.

Kwa hiyo unaweza kuona hawa wanaowatetea nao ni majipu. Tutaanza kuwafuatilia. Hata ukimtoa huyo, nikimsema hadharani wanasema eti nimefanya kosa.”

Rais Magufuli alisema kwa bahati nzuri aliwateua yeye na kuwatangaza hadharani, hivyo akahoji sababu za kutotangazwa hadharani siku ya kutenguliwa kwa kuwa ndiyo saizi yake aliyewateua.

Kama ni mkurugenzi wa manispaa au wa wapi nimemteua mimi. Eti wanasema apewe muda wa kujieleza. Ajieleze yeye aliwapa muda wananchi kujieleza alipokuwa anawaibia? Napenda niwahakikishie tutaendelea kusimama imara,” alisema Dk Magufuli.

Zaidi, msikilize kwenye video Hapo Juu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad