|
Timu ya
Ndanda FC ya mkoani Mtwara imeikazia Azam FC na kuilazimisha sare ya kufungana
magoli 2-2 kwenye mchezo wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara uliochezwa leo
April 06,2016 kwenye uwanja wa Azam Complex, Chamazi.
Azam FC
walianza kupata bao dakika ya 16 kipindi cha kwanza kupitia kwa Ramadhani
Singano ambaye aliunganisha pasi ya Michael Balou kabla ya Didier Kavumbagu
kutupia kambani bao la pili muda mfupi kabla ya kwenda mapumziko.
Mchezaji, Atupele Green alizifungua nyavu za Azam FC kwa
kuusukuma mpira kambani kwa mkwaju wa penati baada ya golikipa wa Azam FC,
Aishi Manula kumwanusha Paul Ngalema kwenye eneo la hatari wakati akijaribu
kuokoa hatari golini kwakwe.
Bao la
kusawazisha la Ndanda FC lilikuwa ni la kujifunga ambapo beki wa Azam FC Agrey
Morris aliugonga mpira uliokuwa unaelekea goli na kuubadilisha mwelekeo kisha
kumshinda golikipa Aishi Manula na kuzama wavuni.
Matokeo hayo
ni habari njema kwa Yanga SC na Simba SC ambazo timu zote hizo tatu zinaongoza
mbio za kuwania ubingwa wa ligi msimu huu.
Matokeo hayo
yanaifanya Azam FC ijiongezee pointi moja na kufikisha 52 baada ya kucheza
mechi 23, wakiwa nafasi ya tatu nyuma ya mabingwa watetezi, Yanga SC wenye
pointi 53 za mechi 22, wakati Simba SC inaongoza kwa pointi zake 57 za mechi
24.
Baada ya mchezo
huo, Azam FC inarejea kambini kujiandaa na mchezo wake wa kwanza hatua ya 16
Bora Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Esperance ya Tunisia Jumapili mjini
Dar es Salaam.
Mchezo
mwingine wa Ligi Kuu leo, wenyeji Majimaji FC wameifunga 2-0 Coastal Union
Uwanja wa Majimaji mjini Songea.
Baada ya
Mechi za Leo, VPL itaendelea tena Jumamosi April 09,2016.
LIGI KUU
VODACOM TANZANIA BARA 2015/2016 –
RATIBA.
Jumamosi
Aprili 09,2016.
Ndanda FC v
Mwadui FC
African
Sports v Kagera Sugar
Mtibwa Sugar
v Tanzania Prisons
Jumapili
Aprili 10,2016.
Mgambo JKT v
Mbeya City
Jumatatu
Aprili 11, 2016.
Toto
Africans v Majimaji
Jumatano
Aprili 13, 2016.
Mtibwa Sugar
v Azam FC
Yanga v
Mwadui FC
Jumamosi
Aprili 16, 2016.
Coastal
Union v JKT Ruvu
Yanga v
Mtibwa Sugar
Jumapili
Aprili 17, 2016.
Simba SC v
Toto Africans
Jumatano
Aprili 27, 2016.
Azam FC v
Majimaji
Yanga v
Mgambo JKT
Jumamosi
Aprili 30, 2016.
Toto
Africans v Yanga
Simba SC v
Azam FC
Ndanda FC v
Kagera Sugar
African
Sports v Coastal Union
Mwadui FC v
Stand United
Mtibwa Sugar
v Mbeya City
|
No comments:
Post a Comment