West Ham
walifufuka na kufunga Bao lao la kwanza Dakika ya 44 kwa Kichwa cha Andy
Carroll alieunganisha krosi ya Cresswell na kupata Bao la Pili Dakika ya 47
kupitia tena Andy Carroll ambae aliunganisha Mpira wa Kona iliyoooshwa na
kumkuta Mark Noble alieurudisha tena Golini na kumkuta Carroll aliepiga Shuti
la kwanza ambalo lilizuiwa na kuachia kigongo cha pili na kumparaza Beki na
kumhadaa Kipa Ospina.
Dakika ya 52
Carroll alipiga Bao la 3 na kukamilisha Hetitriki yake ya ndani ya Dakika 9 tu.
Arsenal
walisawazisha na kuambua Sare ya 3-3 katika Dakika ya 70 kwa Bao la Laurent
Koscielny.
Matokeo haya
yamezibakisha Arsenal Nafasi ya 3 wakiwa Pointi 10 nyuma ya Vinara Leicester
City na West Ham kuwa Nafasi ya 6.





No comments:
Post a Comment