KLABU BINGWA AFRICA:-Yanga SC yaangukia Kombe la Shirikisho barani Afrika. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, April 21, 2016

KLABU BINGWA AFRICA:-Yanga SC yaangukia Kombe la Shirikisho barani Afrika.

Klabu ya Yanga SC imetolewa katika Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kufungwa mabao 2-1 na Al Ahly usiku wa Jana April 20, 2016 kwenye mchezo wa Ligi hiyo  Uwanja wa Borg El Arab mjini Alexandria katika mchezo wa marudiano hatua ya 16 Bora.

Al Ahly inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 3-2 baada ya awali kulazimisha sare ya 1-1 Uwanja wa Dar es Salaam wiki mbili zilizopita.

 Donald Ngoma aliifungia bao la Yanga dakika ya 67’’ 

Kwa mujibu wa kanuni za CAF, timu zilizotolewa kwenye hatua ya 16 bora ya michuano ya mabingwa Afrika, zinakutana na timu washindi wa wa hatua ya 16 bora kutoka kombe la sirikisho.

 Kwa maana hiyo, Yanga SC inaangukia katika michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad