KOMBE LA SHIRIKISHO:-Azam FC yatupwa kwa kufungwa mabao 3-0 na Esperance. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, April 20, 2016

KOMBE LA SHIRIKISHO:-Azam FC yatupwa kwa kufungwa mabao 3-0 na Esperance.

Kipa wa Esperance, Moez Ben Cherifia akidaka mpira wa juu dhidi ya mshambuliaji wa Azam FC, John Bocco.

Mabingwa wa kombe la Kagame timu ya Azam FC, imekukubali kichapo cha magoli 3-0 dhidi ya Esparance ya Tunisia,katika Mechi yao ya pili ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya Mashindano ya CAF ya Kombe la Shirikisho na kutupwa nje ya Mashindano hayo.
Nahodha wa Azam FC, John Bocco akiwafungva tela wachezaji wa Esperance leo Uwanja wa Olimpiki Novemba 7, mjini Rades, Tunis.

Azam FC, ambao walishinda 2-1 katika Mechi ya Kwanza iliyochezwa huko Azam Complex, Chamazi ,Jijini Dar es Salaam wiki mbili  zilizopita, Jana,April 19, 2016 walipigwa Bao zote 3 katika Kipindi cha Pili.

Bao hizo zilifungwa Dakika za 49, 64 na 81 na Saad Bguir, Haythem Jouini na Fakhreddine Ben Youssef.
Hivyo Azam FC wametupwa nje ya Mashindano haya na ES Tunis kusonga mbele kwa Jumla ya Mabao 4-2 .

Huu ni mwaka wa tatu Azam FC wanashiriki michuano ya kimataifa lakini wameshindwa kufika hatua ya robo fainali.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad