|
Rais wa
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Dkt. Ali Mohamed Shein.
RAIS wa
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Dkt. Ali Mohamed Shein leo Jumamosi,
April 9, 2016 ametangaza Baraza la Mawaziri litakalosimamia kazi za serikali
kwa kipindi cha uongozi wake wake kwa mujibu wa sheria.
Dkt. Shein
amesema amepunguza ukubwa wa baraza hilo kutoka Wizara 16 hadi kuwa Wizara 13
zenye Mawaziri ni 13 na Manaibu Waziri 7, ambapo wizara tatu amezivunja na
kuzigawa ndani ya hizo Wizara 13 za sasa.
Ameongeza
kuwa, mawaziri aliowatangaza leo atawaapisha kesho Jumapili asubuhi katika
Viwanja vya Ikulu visiwani Zanzibar.
Baraza la
Mawaziri Zanzibar hao ni;
1). Ofisi ya
Rais na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi – Issa Haji Ussi Gavu.
2). Katiba
na Sheria Utumishi wa Umma – Haroun Ali Sleiman.
3). Tawala
za Mikoa na Idara maalum – Haji Omari Kheir.
4). Makamo
wa 2 wa Rais – Mohd Aboud.
5). Waziri
wa Fedha na Mipango – Dk. Khalid Salum Mohd.
6). Afya –
Mahmoud Thabit Kombo.
7). Wizara
ya Elimu – Riziki Pembe Juma.
8). Viwanda
na Masoko – Amina Salum Ali.
9). Ujenzi,
Mawasiliano na Uchukuzi – Ali Karume.
10). Habari
Utalii Utamaduni na Michezo – Rashid Ali Juma.
11). Kilimo
Maliasili Mifugo na Uvuvi – Hamad Rashid Mohd.
12).
Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto – Mauldine Castiko.
13). Maji
Ardhi Nishati na Mazingira – Salama Aboud Talib.
|
No comments:
Post a Comment