Tunda la
tikitimaji lina kiwango kikubwa cha Lycopene kuliko tunda lolote au mboga za
majani.
Ndani ya
tunda hili kuna madini ya Potasium.
Lina uwezo mkubwa wa kusaidia misuli na
mfumo wa fahamu kwa ujumla kufanya kazi zake vizuri.
Tikitimama
pia lina Amino Asidi na virutubisho vingine vinavyosaidia kurahisisha mtiririko
wa damu kwenye mishipa yake.
Sifa ya
kipekee iliyopo katika tunda hili ni ule uwezo wake wa kusaidia kupunguza ama
kuondoa tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.
Kwa kunywa juisi yake
iliyokamuliwa bila kumenywa kwa maganda yake, kutaisadia kabisa kuondoa tatizo
hilo.
Tunda hili
limeonesha kulainisha vizuri mishipa ya damu na kufanya mzunguko wa damu
mwilini kuwa mwepesi bila athari yoyote mbaya.
Kwenye
tikitimaji kuna faida tangu kwenye majani, ganda na tunda na hata nyama yake.
Potassium
iliyomo kwenye tikitimaji, huimarisha misuli ya mwili na huwafaa sana
wanamichezo. Ulaji wa kipande kimoja baada ya kufanya mazoezi, huondoa tatizo
la kukaza kwa misuli ya miguu, pia husaidia kupunguza uzito mwilini.
Tikitimaji
lina kiwango kidogo sana cha kalori lakini lina kiwango kikubwa cha maji, hivyo
kwa mtu anayetaka kupunguza uzito wa mwili linaweza kumsaidia kwa kula kwa
wingi ambapo atakuwa anajisikia tumbo kujaa lakini bila kuwa ameshiba sana,
hivyo kuwa rahisi kwake kujizuia na kula vyakula vingine hata kwa kutwa nzima
na bila kuathirika kiafya.
Kirutubisho
cha ‘Arginine’ kilichomo kwenye tikitimaji huchochea kwa kiasi kikubwa
uimarishaji wa kinga ya mwili.
Huondoa sumu mwilini, vilevile hufanya kazi
muhimu ya uponyaji vidonda na kuondoa ‘Ammonia’ na sumu nyingine mwilini ambazo
zinapozidi humfanya mtu kusikia uchovu na kusababisha ugonjwa wa ini na figo.
Tikitimaji
pia hufaa kuliwa na wagonjwa wa presha kwani hushusha shinikizo la juu la damu,
huongeza nuru ya macho, hutoa kinga kubwa dhidi ya magonjwa nyemelezi yakiwemo
yale hatari kama vile kansa ya matiti, kibofu cha mkojo, mapafu na kansa ya
tumbo.
|
Tuesday, March 15, 2016
ZIJUE FAIDA:-Ni za Tikitimaji Mwilini Mwako.
Tags
# DONDOO
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
DONDOO
Labels:
DONDOO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment