Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amesema jumla ya
wafanyakazi 202 katika halmashauri 14 katika mikoa ya Singida na Dodoma
waligundulika kuwa hewa na kulipwa mishahara kila mwezi.
Rais
ameyasema hayo alipokuwa akiwakumbusha wakuu wa Mikoa wapya ambao amewaapisha rasmi leo,March 15,2016, Ikulu jijini Dar es salaam.
''Kwa mikoa
miwili tuu wafanyakazi hao 202 wanalipwa mishahara hewa na kwenye data
ilionyesha wengine wamefariki, wamestaafu, wamefukuzwa , wengine likizo bila
malipo wote hao kumbe wanalipwa malipo ya serikali fedha ambazo zingetumika
kutatua matatizo ya wananchi''.Amesema Rais Magufuli.
Kwa msingi
huo kwa halmashauri 180 nchini ina maana kwa mahesabu ya haraka haraka kuna
wafanyakazi 2000 na zaidi wanalipwa mishahara hewa.
Hivyo Rais
Dkt Magufuli ametoa agizo kwa wakurugenzi wa taasisi za serikali kuanzia leo
ndani ya siku 15 kuhakikisha wanapitia majina ya waajiriwa wote wa serikali na
kuondoa majina ya ambao wanalipwa bila kufanya kazi.
Hapa chini ,Tazama
Video hii Kumsikiliza Rais Magufuli Akiongea na Wakuu hao wapya wa Mikoa.
|
No comments:
Post a Comment