TRAFFIC DAR:-Wakusanya Milioni 577 za Makosa Barabarani ndani Ya Siku 12 Tu. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, March 19, 2016

TRAFFIC DAR:-Wakusanya Milioni 577 za Makosa Barabarani ndani Ya Siku 12 Tu.

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam kupitia kitengo chake cha Usalama Barabarani limekamata magari mbalimbali kwa makosa ya Usalama barabarani.

Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro aliwaambia waandishi wa habari jana ,March 18, 2016,kuwa Jumla ya Tshs. 577,831,000 zimekusanywa ikiwa ni tozo kwa makosa hayo kwa mida wa siku 12, kuanzia 07/03/2016 hadi tarehe 18/03.2016.
Kamanda Sirro amewataka Madereva kuwa makini na waangalifu pindi wawapo barabarani ili kuepuka adhabu zitolewazo ili vipato hivyo viwasaidie katika maisha yao ya kila siku.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad